WAKATI Arsenal wakitinga hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupata ushindi nyumbani, Liverpool imejikuta ikibanwa ugenini kwa kuambulia sare.
Arsenal walipata ushindi muhimu nyumbani dhidi ya Borussia Dortmund kwa kuwalaza mabao 2-0 wakati Liverpool ililazimishwa sare ya 2-2 na Ludogorets .
Mabao ya Yaya Sanogo na jingine la Alexis Sanchez yalitosha kuivusha Arsenal hatua hiyo katika mechi kali iliyochezwa uwanja wa Emirates.
Arsenal imeungana na Wajerumani hao kutinga hatua ya 16 Bora kutoka kundi D baada ya kufikisha pointi 10, tatu nyuma ya Dortmund inayoongoza kileleni.
Nao Liverpool ililazimishwa sare ya 2-2 na Ludogoretsna kuzidi kujiweka pabaya katika azma yao ya kucheza hatua ya mtoano.
Ludogorets waliwashtukiza wageni wao kwa kupata bao la mapema la dakika tatu kupitia Dani Abalo kabla ya Liverpool kusawazisha dakika tano baadaye kupitia Rickie Lambert na baadaye Jordan Henderson kuwapa uongozi wa 2-1 wageni.
Hata hivyo Vijogoo vya England walishindwa kulinda bao lao baada ya kuruhusu wenyeji kusawazisha dakika mbili kabla ya mchezo huo kumalizika baada ya Georgi Teziev kuifuingia Lodogorets.
Sare hiyo imeifanya Liverpool kufikisha pointi nne na kushika nafasi ya tatu ikitanguliwa na Basel iliyolazwa bao 1-0 na Real Madrid iliyotangulia 16 Bora ikiongoza kundi B.
Bao la Real lilifungwa na Ronaldo na kumfanya Mreno huyo kumfikia Raul katika orodha ya waliofunga mabao mengi katika ligi hiyo wakishika nafasi ya pili nyuma ya Lionel Messi anayeongoza kwa mabao 74 dhidi ya 71 na wakali hao.
Bao la Real lilifungwa na Ronaldo na kumfanya Mreno huyo kumfikia Raul katika orodha ya waliofunga mabao mengi katika ligi hiyo wakishika nafasi ya pili nyuma ya Lionel Messi anayeongoza kwa mabao 74 dhidi ya 71 na wakali hao.
Katika mechi nyingine Zenit iliitambia Benfica kwa kuilaza bao 1-0, huku Atlético Madrid ikiendeleza rekodi yao ya kutofungwa uwanja wa nyumbani kwa kuicharaza Olympiakos Pirates kwa mabao 4-0 na kufuzu 16 Bora.
Wakali wa Italia, Juventus wakipata ushindi muhimu ugenini dhidi ya Malmo, huku Monaco ikiwa ugenini ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bayer Leverkusen, huku Anderlecht ikiinyoa Galatasaray kwa mabao 2-0.
Mpaka sasa wakati michuano hiyo ikisaliwa na raundi moja kabla ya kufikia tamati hatua ya makundi timu nane ndizo zimejihakikisha hatua inayofuata zitakazochezwa mwezi ujao.
Timu hizo ni pamoja na Atletico Madrid, Real Madrid na Barcelona zote za Hispania, Chelsea na Arsenal za England, Bayern Munich na Borussia Dortmund za Ujerumani, PSG ya Ufaransa, POrto ya Ureno na Shakhtar Donetsk ya Uturuki.
No comments:
Post a Comment