RAIS wa CECAFA, Leodgar Tenga akiwa na Katibu wake, Nicolaus Musonye |
Baraza
la vyama vya soka Afrika mashariki na kati (CECAFA) kwa sasa linaangalia
uwezekano wa kupata muandaaji mpya wa michuano ya mwaka huu 2014 ya
chalenji kufuatia Ethiopia kujitoa.
Katibu
mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye amenukuliwa toka Nairobi, Kenya kuwa Ethiopia imejitoa kuandaa michuano hiyo.
“Ethiopia
imetuandikia na kusema hawako katika nafasi ya kuandaa michuano hiyo,”
Musonye amesema na kuongeza kuwa CECAFA imekubali kujitoa kwao
“Hatuna la kufanya zaidi ya kukubali ombi la lakini tayari tumeanza kazi ya kusaka mwenyeji mpya.”
Musonye
amethibtisha hilo licha ya shirikisho la soka la Ethiopia EFF
kuwaandikia wakiwa wamechelewa, lakini amesema kuwa michuano hiyo
itafanyika kwa tarehe iliyotajwa kati ya Novemba na Desemba na kwamba
mwenyeji mpya atatangazwa wiki iyayo.
"Sudan yuko tayari akingojea hivyo michuano inaweza kuelekea Khartoum, lakini tutatangaza baadaye wiki ijayo"
Mwaka uliopita 2013 michuano
hiyo ilifanyika nchini Kenya ambapo wenyeji walitwaa taji hilo baada ya
kuifunga Sudan katika mchezo wa fainali uliopigwa katika dimba la Nyayo
jijini Nairobi.
No comments:
Post a Comment