Meshack Abel alipokuwa Bandari Fc |
Wawa |
USAJILI wa dirisha dogo msimu wa 2014/2015 umefungwa rasmi jana (Desemba 15 mwaka huu) huku
wachezaji 15 kutoka nje wakiombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kutoka
nchi mbalimbali.
Wachezaji
walioombewa ITC kwa timu za Ligi Kuu ni Abdulhalim Humoud kutoka Sofapaka ya
Kenya kwenda Coastal Union, Brian Majwega kutoka KCC (Uganda) kwenda Azam na
Castory Mumbara kutoka Three Star Club (Nepal) kwenda Polisi Mara.
Wengine ni Charles
Misheto kutoka SP Selbitiz (Ujerumani) kwenda Stand United na Chinedu Michael
Nwankwoeze kutoka Nigeria kwenda Stand United.
Pia wamo Dan
Serunkuma kutoka Gor Mahia (Kenya) kwenda Simba, Emerson De Oliveira Neves
Roque kutoka Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Bonsucesso FC (Brasil)
kwenda Yanga, Halidi Suleiman kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United na
Juuko Murushid kutoka SC Victoria University (Uganda) kwenda Simba.
Wachezaji wengine ni Kpah
Sean Sherman kutoka Aries FC (Liberia) kwenda Yanga, Meshack Abel kutoka KCB
(Kenya) kwenda Polisi Morogoro na Moussa Omar kutoka Flambeau (Burundi) kwenda
Stand United.
Pia wamo Nduwimana Michel kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United,
Serge Pascal Wawa kutoka El Merreikh (Sudan) kwenda Azam na Simon Serunkuma
kutoka Express FC (Uganda) kwenda Simba.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF inatarajia kukutana hivi karibuni kwa
ajili ya kupitia usajili wa wachezaji wote walioombewa katika dirisha dogo
wakiwemo wale wa mkopo.
No comments:
Post a Comment