RAIS Jakaya Kikwete anasubiriwa kwa hamu na watanzania kukata kiu juu ya baadhi ya mambo yaliyojiri nchini ambayo yameliacha taifa kwenye sintifashamu.
Sakata la uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow zipatazo bil. 306, na mvurugano uliojitokeza kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ni kati ya vinavyosubiriwa kusikia Rais atasema nini.
Juzi watanzania walidokezwa kuwa kungekuwa na fursa kwa Rais kuzungumza na wananchi kabla ya kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu kukanusha taarifa hizo na kudai Rais atazungumza na Watanzania kesho kupitia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.
Je mawaziri waliotajwa kuhusika kwa namna moja juu ya sakata ya Escrow na uchaguzi wa serikali za mitaa waenda na maji au watapeta kulingana na duru za kisiasa na kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaigana kwamba hatajiuzulu na pia yeye na Rais wametoka mbali?
Ngoja tusubiri tuone Rais atakata kiu ya watanzania kivipi hiyo kesho katika hotuba yake!
No comments:
Post a Comment