Kikosi cha Simba kitakachokuwa mjini Shinyanga, |
Azam watakuwa uwanja wa nyumbani wa Chamazi |
Kikosi cha Yanga kilichopo ugenini jijini Mbeya kuvaana na Mbeya City |
Vinara Yanga wenyewe watakuwa kwenye uwanja wa Sokoine kwa mara nyingine tena kupepetana na wenyeji wao Mbeya City, ikiwa ni siku chache baada ya kugawa dozi ya mabao 3-0 dhidi ya Prisons.
Simba walioanza kushika kasi katika ligi hiyo baada ya kuchechemea kwa muda mrefu, pia ipo ugenini mkoani Shinyanga kwa ajili ya kupepetana na Stand United kwenye uwanja wa Kambarage.
Mabingwa watetezi Azam watakuwa uwanja wa nyumbani wa Azam Complex, Chamazi kuikaribisha Prisons-Mbeya baada ya katikati ya wiki kubanwa mbavu na Ruvu Shooting na kutoka suluhu ya 0-0.
Yanga watakuwa na hamu ya kuendeleza rekodi yao ya kushinda mfululizo, ingawa Mbeya City ambayo imekuwa haina msimu mzuri safari hii ikiwa imeapa kumaliza uteja kwa wapinzani wao hao.
Mbeya City iliyopanda ligi kuu msimu uliopita, haijawahi kuifunga Yanga zaidi ya kulazimisha sare au kuambulia vipigo, kitu ambacho Kocha wake, Juma Mwambusi anaamini leo watavunja mwiko.
Hata hivyo Yanga imetamba kutaka kutoa dozi kwa lengo la kuongeza morali kabla ya kuondoka nchini kwenda Botswana kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI.
Yanga inayoongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 28, mbili zaidi ya Azam yenye 26 itarudiana na BDF wiki ijayo mjini Gaborone baada ya wiki iliyopita kuwacharaza mabao 2-0.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema hawaoni cha kuwazuia kuvuna pointi nyingine tatu jijini Mbeya wakati kikosi chao kimeandaliwa vema na kina morali mkubwa.
Muro alisema anafahamu Mbeya City ni timu ngumu na itataka kutumia vema uwanja wa nyumbani, lakini Yanga imejipanga kutoka na pointi zote ili kujikita zaidi kileleni kabla ya kwenda Botswana.
Wakati Yanga na Mbeya wakiwindana hivyo, Simba wenyewe wakiwa na furaha ya ushindi wa mabao 2-0 iliyopata ugenini mjini Morogoro dhidi ya Polisi wataivaa Stand United wakiwa na tahadhari kubwa.
Stand Utd imetoka kuwatoa nishai Mgambo JKT kwa kuicharaza mabao 4-1, kitu ambacho kinaonyesha namna gani wameanza kuizoea ligi hiyo wanayoicheza kwa msimu wao wa kwanza.
Katika pambano hilo kila timu itakuwa ikitegemea nyota wake, Simba ikitambia akina Emmanuel Okwi, Dan Sserunkuma, Eliasi Maguri na wengine huku Stand ikimtegemea Mnigeria Abasalim Chiibibele na Heri Mohammed wenye mabao manne kila mmoja katika ligi hiyo.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Oktoba 4, mwaka jana timu hizo zilizoshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye uwanja wa Taifa.
Angalia msimamo wa Ligi Kuu ulivyo:
P W D L F A GD Pts
01. Yanga 14 08 04 02 18 07 11 28
02. Azam 14 07 05 02 22 12 10 26
03. Kagera Sugar 16 06 06 04 13 11 02 24
04. Simba 14 04 08 02 15 11 04 20
05. Ruvu Shooting 15 05 05 05 10 11 -1 20
06. Mtibwa Sugar 15 04 07 04 15 15 00 19
07. Coastal Union 16 04 07 05 11 11 00 19
08. Polisi Moro 16 04 07 05 12 14 -2 19
09. JKT Ruvu 15 05 04 06 14 15 -1 19
10. Ndanda Fc 16 05 04 07 14 18 -4 19
11. Mbeya City 14 04 05 05 09 11 -2 17
12. Mgambo JKT 14 05 02 07 08 15 -7 17
13.Stand Utd 15 03 06 06 13 18 -5 15
14. Prisons 14 01 08 05 10 15 -5 11
Wafungaji:
8- Didier Kavumbagu(Azam)
7- Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
6- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ame Ali (Mtibwa), Simon Msuva (Yanga),
5-Danny Mrwanda (Yanga), Kipre Tchetche (Azam)
4- Rama Salim (Coastal), Emmanuel Okwi (Simba), Nassor Kapama, Jacob Massawe (Ndanda), Heri Mohammed, Abasalim Chiibibele (Stand Utd) , Malimi Busungu (Mgambo)
3- Ally Shomari (Mtibwa), Frank Domayo (Azam), Atupele Green (Kagera)
2- Shaaban Kisiga, Dan Sserunkuma, Elias Maguli (Simba), Salum Kanoni, (Kagera Sugar) Aggrey Morris (Azam), Najim Magulu, Jabir Aziz (JKT Ruvu), Amissi Tambwe, Jerry Tegete, Mrisho Ngassa, Andrey Coutinho (Yanga), Ibrahim Kihaka (Prisons), Mussa Mgosi (Mtibwa), Mussa Said (Stand Utd), Ally Nassor (Mgambo), Nicolaus Kabipe (Polisi),Yahya Tumbo (Ruvu Shooting)
No comments:
Post a Comment