Hazard akiifungia Chelsea bao pekee dhidi ya West Ham |
Sanchez wa Arsenal akishangilia bao la pili alilolifunga yeye wakati wakiizamisha QPR |
Silva akiwatungua Leichester City |
Ashley Young akifunga bao la 'jioni' kuipa ushindi murua Manchester City ugenini dhidi ya Newcastle Utd |
Arsenal ikiwa uwanja wa ugenini nyumbani kwa QPR ilipata mabao hayo katika kipindi cha pili na kuizamisha wenyeji wao kwa mabao 2-1, huku Chelsea nao wakipata ushindi ugenini mwa West Ham United kwa bao 1-0 bao lililofungwa Eden Hazard akimalizia kazi ya Ramires.
Katika pambano la Arsenal na QPR, Giroud alianza kuifungia timu yake bao dakika ya 64 kabla ya dakika nne baadaye Sanchez kuongeza la pili na wenyeji kuja kupata la kufutia machozi dakika ya 82 kupitia kwa Charlie Austin.
Kwa ushindi iliyopata Chelsea imeifanya mabingwa hao wa Kombe la Ligi kufikisha pointi 63, huku wapinzani wao wakisaliwa na pointi 39 na kukamata nafasi ya 10 huku Arsenal wakiwafukuzia mabingwa watetezi Manchester City waliopo nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 54.
City wenyewe alipata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Leicester City na kuwqafanya wafikishe pointi 58 baada ya kushuka dimbani mara 28. Mabao ya washindi yaliwekwa kimiani na David Silva na James Milner.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Liverpool ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burnley, Manchester United ikiwa ugenini ilipata ushindi muhimu wa bao 1-0 mbele ya Newcastle United, huku Stoke City ikiitambia Everton kwa kuilaza mabao 2-0 na Tottenham Hotspur ilipata ushindi mujarabu kwenye uwanja wake wa nyumbani wa White Hart Lane kwa kuilaza Swansea City kwa mabao 3-2.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena keshokutwa kwa pambano moja tu kati ya QPR dhidi ya Spurs na timu nyingine zitakuwa kwenye majukumu ya Kombe la FA kabla ya ligi hiyo kuendelea wikiendi ijayo ya Machi 14 na 15.
No comments:
Post a Comment