LEO ndiyo Leo wakati wanaume 22 wa klabu za Manchester United na Arsenal watakapovaana katika pambano kali la Ligi Kuu ya England, huku kila timu ikihitaji ushindi ili angalau kujihakikisha nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo.
Pambano hilo litakalopigwa kwenye Uwanja wa Emirates limevuta hisia kali za mashabiki kutokana na ukweli timu zote zilipata matokeo tofauti katika mechi zao zilizopita. Arsenal inaifuata Mashetani Wekundu wakiuguza kichapo cha bao 1-0 walichopewa nyumbani na Swansea City wakati Mashetani hao wakichekelea ushindi wa ugenini dhidi ya Crystal Palace.
Arsenal waliopo nafasi ya tatu watahitaji ushindi huku wakiiombea mabaya waliokuwa mabibngwa watetezi manchjester Citrty watakaokuwa ugenini kuumana na Swansea kusudi warejeshe tumaini ya kukamata nafasi ya pili, nafasi kubwa kwa klabu hiyo kwa hivi karibuni kama wataipata mwisho wa msimu.
Mashetani wanaokamata nafasi ya nne nyuma ya Arsenal itakuwa ikihitaji ushindi ili kuipiku Wapiga Mitutu hao kwa tofauti ya pointi moja na kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kurejea kwenye namba za juu ambazo msimu uliopita walizisikia redioni.
Mechi ya leo inakumbushia Robo Fainali ya Kombe la FA lililochezwa mwezi Machi na Arsenal kuwatoa nishai wapinzani wao kwa mabao 2-1.
Ukiachana na pambano hilo la leo, matokeo ya mechi zilizochezwa wikiendi hii ni kama ifuatavyo;
Liverpool ikiwa nyumbani ilikwanguliwa mabao 3-1 na Crystal Palace, huku
Southampton ikitafuna Aston Villa kwa mabao 6-1.
Matokeo ya mechi nyingine ni kama ilivyo hapo chini;
Burnley 0-0 Stoke
Queens Park Rangers 2-1 Newcastle United
Sunderland 0-0 Leicester City
Tottenham Spurs 2-0 Hull City
West Ham 1-2 Everton
No comments:
Post a Comment