Wanachuo wa KIU Tanzania wakiwa katika maandamano hayo ya hivi karibuni |
WANAFUNZI WA KITIVO CHA SAYANSI YA
TIBA CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA CHA KAMPALA, GONGO LA MBOTO DAR ES SALAAM
Kutokana na
matatizo mbalimbali ya chuo kikuu kishiriki cha Kampala, ambayo yamesababisha
kuwa na migomo ya mara kwa mara katika kitivo cha afya. Na yamefikishwa katika
ngazi mbalimbali za uongozi wa serikali ikiwemo wizara ya Elimu, wizara ya Afya
na Bunge.
MATATIZO:
Chuo chetu kinakabiliwa na matatizo
mengi ambayo kwa namna moja au nyingine yanarudisha nyuma maendeleo ya
wanafunzi kimasomo, matatizo hayo ni kama ifuatavyo;
1. Kutokusajiliwa kwa kada zote za afya
katika bodi husika za afya nchini ( ambazo zinatolewa chuoni hapa.
Kada ya udaktari, ufamasia na maabara
hazina usajili wa bodi husika zinazosimamia taaluma hizo zikiwemo pharmacy
council, Tanganyika medical association na medical laboratory council na NACTE
(kwa wanafunzi wa diploma na certificate). Kutosajiliwa kwa kada hizo
kunapelekea wanafunzi wanaohitimu chuoni hapo kutotambulika hivyo kupelekea
kukosa ajira.
2. Kusimamishwa masomo kwa wanafunzi 5
bila sababu za msingi na kupewa kesi ambazo
hawajasifanya
3. Kiwango kikubwa cha ada(tuition fee)
Kikao cha tarehe 13/11/2014
kilichofanyika wizara ya elimu kilitoa mapendekezo ya kupunguza ada kwa chuo
cha kampala lakini hakuna utekelezaji mpaka sasa. Kwa mfano kwa mwaka wa masomo
2013/2014 wanafunzi wa kada ya ufamasia wa ngazi ya shahada wanalipa tsh
5,400,000/=. Wakati wale wa mwaka wa masomo 2014/2015 wanalipa ada kiasi cha
tsh 3,800,000/=. Kwa wanafunzi wa kada ya udaktari ngazi ya shahada mwaka wa
masomo 2013/2014 wanalipa tsh 9,900,000/=. Wakati wa mwaka wa masomo 2014/2015
wanalipa kiasi cha tsh 6,700,000/=. Kwa wanafunzi wa stashahada ya
udaktari,famasi na maabara wanalipa kiasi cha tsh 1,900,000/=.
4. Mtaala wa kufundishia(curriculum).
Chuo chetu kinatumia mtaala tofauti
na ule wa Tanzania(wa Uganda) ambao unawapa ugumu baraza husika kukisajili chuo
chetu. Mtaala huo pia unawapa kazi sana wanafunzi katika kufuatilia na
kuyaelewa yale wanayofundishwa kwan umebeba masomo mengi kwa muhula mmoja kwa
mfano wanafunzi wa shahada ya ufamasia wanasoma masomo 11 kwa muhula mmoja
katika chuo chetu wakati ni tofauti ukilinganisha na vyuo vingine ambavyo kwa
muhula mmoja wanasoma masomo 4 hadi 5. Kwa wanafunzi wa stashahada wanasoma
hadi masomo 15 kwa muhula mmoja ambayo kwa hali ya kawaida huwezi kuyamudu kwa
wakati.
5. Utaratibu wa supplementary.
Supplementary zinafanyika kila baada
ya muhula wa masomo na kwa kila somo mwanafunzi anawajibika kulipia tsh
40,000/= wakati ukilinganisha na vyuo vingine supplementary zinafanyika mwisho
wa mwaka wa masomo na mwanafunzi halipii kabisa au kuchanga kiasi kidogo sana
kwa ajili ya mitihani hiyo. Pia mwanafunzi anawajibika kurudia muhula endapo
atafeli mtihani wake wa supplementary hata kama ni somo moja tu na atalazimika
kurudia masomo yote hata yale ambayo alifaulu vizuri.
6. Uongozi mbovu wa kitivo cha sayansi
ya afya(health science).
Uongozi wetu hauna mfumo unaoeleweka
wa utoaji matokeo ambapo katika mtihani mmoja mwanafunzi anapokea matokeo yake
mara tatu tofauti. Kutokuonekana kabisa kwa matokeo ya baadhi ya wanafunzi hii
inachangiwa pia na mfumo wa utoaji matokeo hayo ambapo mpaka leo hii wanafunzi
wa chuo wanabandikiwa matokeo ubaoni kama wanafunzi wa shule ya msingi. Pia
uongozi hauna mazoea wala utaratibu wa kumsikiliza mwanafunzi.
7. Uhaba wa miundombinu ya chuo.
Chuo chetu kinakabiliwa na uhaba
mkubwa wa vifaa vya ufundishaji na ujifunzaji hasa maabara, vingine ni kama
projector na microphone ambapo utakuta darasa la watu zaidi ya 100 halina
microphone na kuoelekea baadhi ya wanafunzi kuhudhuria darasani bila kupata
chochote kutokana na kutokumsikia kabisa mwalimu. Pia Chuo hakina usafiri wa
uhakika kwa ajili ya medical rotation na research mbalimbali.
8. Ada ya TCU.
Chuo chetu kina utaratibu wa kuwaibia
wanafunzi wa stashahada na astashahada kwa kuwalipisha kiasi cha tsh 20,000/=
kama ada ya usajili wa TCU wakati TCU wala hawahusiki na wanafunzi hao.huu ni
wizi wa dhahiri kwani hizo fedha wanalipa kupitia account ya chuo na sio TCU.
9. Ukosefu wa uwiano kati ya wafanyakazi
wa chuo.
95% ya wafanyakazi wa chuo chetu ni
wageni na sio watanzania hivyo kupelekea hata matatizo yetu kutopata suluhu na
uangalizi wa karibu kwani wengi wa wafanyakazi hao hawajali hali halisi ya
watanzania.
10. Pesa maalumu kwa ajili ya kada
mbalimbali(special faculty requirement).
Kutokana na majibu yaliyotolewa
katika kikao kilichofanyika tarehe 04/05/2015 kati ya uongozi wa chuo na bodi
ya mikopo ya elimu ya juu(HESLB) imeelezwa kwamba chuo chetu kinakosa fedha
hizo kutokana na kukosa usajili wa kudumu.
11. Masomo ya pre entry(MPP)
Chuo chetu kina utaratibu mbovu wa
kuwafundisha masomo ya sekondari wanafunzi wa shahada wanaochaguliwa chuoni
hapa na masomo hayo hufundishwa kwa muhula mzima na kupelekea kuongezeka muda
wa kuhitimu masomo yao huku wakilipa ada ile ile. Hai hii hupelekea wanafunzi
kuwa na muda mfupi wa likizo kwa ajili ya recessive semester ambayo wanafidia
muda waliosoma masomo ya sekondari(MPP) badala ya course husika.
12. Muda wa kuhitimu masomo``
Wanafunzi wa shahada wameongezewa
muda wa kukaa chuoni hii ni kutokana na urasimu wa chuo na uwepo wa masomo ya
pre entry au MPP ambapo mwanafunzi wa kada ya maabara anatakiwa kusoma kwa
miaka 4.5 badala ya miaka 3 na kada za udaktari na ufamasia wameongezewa miezi
6 ambapo madaktari wanasoma miaka 5.5 badala ya miaka 5 na wafamasia wanasoma
miaka 4.5 badala ya miaka 4 kitu ambacho ni kinyume kabisa na utaratibu wa
elimu ya Tanzania.
13. BRIDGING COURSE NA UDAHILI WA
WANAFUNZI KINYUME NA UTARATIBU.
Kumekua na udahili wa moja kwa moja wa wanafunzi wasio kua na
vigezo katika chuo hiki kinyume na utaratibu,wakifundishwa masomo ya bridging
course ambayo ni kinyume cha sheria,ambayo pia haipo chuo chochote Tanzania na
ilikua ni moja ya sababu zilizo pelekea chuo cha tiba cha IMTU mwaka 2014
kufungiwa. Je,serikali inakiwajibisha
vipi chuo hiki ambacho kinakwenda kinyume na taratibu hizo pamoja na wanafunzi
ambao wizara imethibitisha mbele ya waziri kua haitawasajili,chuo kinawafidia
vipi wanafunzi hao?
14. Ukosefu wa prospectus na university
calendar,
Chuo
hakina prospectus wala university calendar
inayowaongoza wanafunzi na wafanyakazi kwa ujumla na kuwaonyesha ratiba
na matukio ya mwaka mzima.
15. Kudahiliwa katika chuo cha nje ya
nchi wakati tumeomba kama wanafunzi wa ndani ya nchi na tunapata mkopo
tukitambulika kama wanafunzi wa ndani ya nchi, hii inatuletea shida ya
kutambulika kama wanafunzi wa kigeni na kutakiwa ku verify vyeti vyetu kabla ya
kuajiriwa nchini kwetu tofauti na vyuo vingine vilivyopo nchini ambavyo vipo chini ya TCU.
MAJIBU
YA WAZIRI WA ELIMU MUHESHIMIWA SHUKURU KAWAMBWA
Baada ya wanafunzi wa kitivo cha
sayansi ya tiba katika chuo kikuu kishiriki cha Kampala kukumbwa na matatizo
mbalilmbali ambayo yameshindwa kutatuliwa katika ngazi mbalilmbali mpaka pale
yalipofikishwa katika bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania na kuundwa kamati
ili kuweza kushugulikiwa matatizo hayo .
kamati ilipewa muda wa wiki moja kuweza
kukamilishwa kwa kazi hiyo tarehe 4 mwezi huu wa sita leo hii
ni wiki moja imepita na kamati hii haijafika.
Lakini cha kushangaza tulipata ugeni jana
tarehe 10/06/2015 Mh Shukuru Kawambwa waziri wa elimu nchini ambapo alipanga
kuonana na uongozi wa chuo pamoja na serikali ya wanafunzi bila kuwaona
wanafunzi wenye matatizo husika, ambapo baada ya wanafunzi hao kugundua
walimuomba waweze kuongea nae kuhusu matatizo hayo ambayo yameshindwa kupatiwa
ufumbuzi kwa miaka mingi sasa na muda
huo wanafunzi wote wa kitivo cha sayansi ya afya chuoni hapa tulisimamishwa
masomo kwa siku zisizojulikana kuanzia tarehe 8/06/2015.Na muheshimiwa waziri
alipanga kujibu matatizo ya chuo hicho yasiyopungua 15 kwa muda wa dakika 30
akiwa anadai kwamba anawai ndege kwa ajili ya safari ya saa 12 jioni.
N.B: kuja kwa waziri hakujatatua
tatizo lolote bali kumeongeza matatizo kwa sababu tarehe 1/06/2015 alikiri
mbele ya bunge kuwa matatizo ya chuo kikuu cha kampala hayawezi kutatuliwa na
serikali yake.
MAJIBU YA WAZIRI KUHUSU MATATIZO
HAYO.
1;KUHUSU USAJILI
Waziri alikili wazi kwamba chuo
kimesajiliwa kama chuo cha nje na Tume ya vyuo vikuu Tanzania(T.C.U) Na kudai
kwamba vyuo kama hivyo nchini vipo ambapo alipata kutolea mfano wa vyuo kama vile
Jommo Kenyata university,Aga khan university bila kujali kwamba vyuo hivyo
havipo katika orodha ya vyuo vinavyotambulika na Tume ya vyuo vikuu nchini
Tanzania(T.C.U) .
Hoja za Wanafunzi katika hili
jibu ni kama ifuatavyo.
Sisi kama Watanzania halali wa nchi
yetu tunashangazwa na majibu hayo maana sisi tumeomba kama wanafunzi wa ndani
katika vyuo vitano tulivyopaswa kuomba na kupangiwa masomo hayo na Tume ya vyuo
vikuu Tanzania katika chuo hiki cha Kampala international university ambacho hakifuati kanuni na taratibu za nchi
yetu ya Tanzania.
Lakini hoja iliyokuwa kubwa zaidi hiki
kama ni chuo kilichopata usajili kama chuo cha nje ni kwa nini basi wanafunzi
tunapata mikopo ya serikali kama vyuo vya ndani wakati hii ni kinyume maana
mikopo hutolewa kwa wanafunzi wa ndani tuu na isiwe scholarship kama ilivyo kwa
wale wanaosoma nje za nchi.Ambapo hata hivyo vyuo alivyotolea mfano mheshimiwa
waziri havitambuliki na tume ya vyuo vikuu nchini (T.C.U) pamoja na bodi ya
mikopo ya Elimu ya juu nchini(H.E.S.L.B)
Hata hivyo elimu inayotolewa katika
chuo hiki cha kimataifa hakiendani na vyuo vingine vya kimataifa na hata vya
ndani na sisi wanafunzi wa chuo hiki imepelekea kudharaulika na kuwa na
uwasiwasi na soko la ajira hapo baadae endapo tutamaliza salama katika chuo
hiki ambacho wanafunzi wadai haki tena kwa njia ya amani hunyanyaswa kwa
kusimamishwa masomo ,kupelekwa lumande na kusingiziwa kesi mbalimbali ili
waweze kukwamishwa katika masomo yao.
2; MITAALA YA CHUO HIKI.
Majibu ya waziri huyo mwenye dhamana
ya elimu nchini yameonesha wazi kwamba mitaala hiyo imepitishwa na jopo
wataalam maprofesor wengi kutoka chuo
kikuu cha Dar es salaam(U.D.S.M) na kupitishwa na tume ya vyuo vikuu
nchini(T.C.U)
Na mheshimiwa waziri alipata kuongeza wazi kwa kusema kwamba bodi za
afya yaani ile ya famasia,mahabara na udaktari haziusiki na mambo ya mitaala
bali ni T.C.U peke yake ndio inahusika.
Hoja za wanafunzi kuhusu jibu
hili
Sote tunajua wazi kwamba chuo kikuu
cha Dar es salaam hakina kozi za afya sasa bado tunakosa imani na waziri maana haiwezekani mitaala hii
kutungwa na watu wenye fani tofauti na zile za afya hata wawe maprofesor gani
maana hii kazi inabeba maisha ya watu hivyo basi tunaomba bodi husika kupitisha
mtaala huu.
Pia tukirejea barua kutoka baraza la
famasia iliyotumwa katika chuo hiki yenye Kumbukumbu namba AB/300/312/02/20,ya tarehe 14/04/2015
inaeleza moja ya matatizo ambayo yanafanya chuo hiki kutosajiliwa ni pamoja na
mtaala unaotumika ambao ni kinyume na mtaala wa Tanzania ulioanzishwa kwa mujibu wa sheria ya famasia Cap 311 na pia chuo hiki
kilikumbushwa na TCU suala hili kwa barua yenye kumbukumbu namba TCU/A.40/1/VOL.II/14
ya tarehe 16/12/2014 na hata tarehe 4/6/2015 mbele ya bunge waziri wa afya
alisema wazi kwamba hawawezi kumsajili mwanafunzi yeyote kama mtaala wa chuo
chake haujapitishwa na bodi husika na taaluma inayotolewa na chuo husika iwe
inakubalika.
Matatizo haya tumeweza kuyapitisha
katika ngazi mbalimbali za kiserikali ikiwemo Tume ya vyuo vikuu nchini,bodi
husika,kwa mkuu wa wilaya ya ilala na huko kote hatukupata ufumbuzi wa matatizo
haya mpaka sasa tupo ngazi ya bunge.
Hivyo basi sisi wanafunzi wote wa
kitivo cha sayansi ya tiba katika chuo cha kimataifa kampala tunakiri wazi
kwamba hatuna imani na majibu ya waziri wa elimu mh.Shukuru Kawambwa
HOJA ZA WANAFUNZI WOTE KWA UJUMLA WA KITIVO CHA SAYANSI NA TIBA
1.Uhalali wa hotuba wanazotoa hawa
viongozi zinazopingana kama zile zinazotolewa na waziri wa elimu pamoja na
waziri wa afya mwenye dhamana husika.
2.Kuto kuwepo kwa kwa uthibitisho
sahihi wa juu ya usajili wa kozi husika katika
bodi zake.
3.Matumizi ya nguvu katika
kutatua mambo ya wazi kabisa ambayo ni
muhimu kama vile matumizi ya mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kwa siku ya
tarehe 8/06/2015
4.Bodi ya mikopo inatoaje mikopo
katika chuo kilichosajiliwa kama chuo cha nje
5. Kwanini serikali inaruhusu chuo
cha kimataifa Kampala (K.I.U) kisisimamiwe na
BODI ZA UFAMASIA ,MAHABARA ,na UDAKTARI zenye lengo la kusimamia ubora
wa taaluma ikiwa pamoja na kusimamia
mitaala na kudhibiti viwango vya waalimu
wenye sifa kufundisha kozi za afya nchini kuliko ilivyo hivi
sasa ambapo mitaala haitambuliki na bodi
hizo husika.
SISI KAMA WANAFUNZI WA
CHUO KIKUU CHA KAMPALA TUNALAANI VIKALI
MATENDO
YAFUATAYO TULIYOFANYIWA KATIKA
VIPINDI HIVI VYA MGOMO MPAKA SASA
1.Wanafunzi kufukuzwa chuo kila
wanapodai haki zao ambapo siku ya tarehe 30/04/2015 jumla ya wanafunzi kumi na
sita ambao baadhi yao walikuwa wana kamati ya kufuatilia matatizo haya
walisimamishwa masomo .na tarehe 2/06/2015 jumla ya wanafunzi watano
walisimamishwa masomo kwa madai hayohayo na wanafunzi wapatao takribani 19
walipata kulala mahabusu kwa makosa yasiyoeleweka.
2.polisi kutumia nguvu kutawanya wanafunzi
ambao wamekaa na hawafanyi vurugu zozote na waliotii amri za kipolisi kwa kukaa
chini hii tumeona siku ya tarehe 8/06/2015 ambapo polisi waliwamwagia wanafunzi
maji ya kuwasha na kupiga mabomu na kuleta uvunjifu wa amani ambapo
walisababisha wanafunzi wengi waliumia na wengine bado wapo katika matibabu
mpaka sasa,masomo kusitishwa kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizo karibu na
chuo kutokana na ulipukaji wa mabomu ya machozi vilevile kuathirika kwa
wagonjwa katika kituo cha afya cha gongo la mboto kilicho jirani na chuo.
3.Viongozi mbalimbali wa kiserikali
kuacha matatizo haya mpaka yanafikia hali hii kwamba wanafunzi wanahitimu
taaluma yao na kushindwa kuajiliwa.
4.Tunalaani vikali uongozi wa chuo
hiki kwa kushindwa kufuatilia haya
mapaka yanafika hatua hii.
MATATIZO AMBAYO
HAYAJAFANYIWA UFUMBUZI HADI SASA
1. Mitaala(curriculum) haijarekebishwa
ili ifanane na vyuo vingine. Ref. TCU reg no. 40 ibara A uk. 17, reg no. 47 uk.
20 na reg no. 62 uk. 25
2. Kukosekana kwa kalenda inayomuongoza
mwanafunzi kwa mwaka mzima na kumuonesha utaratibu na ratiba za chuo mpaka sasa.
3. Waalimu wengi wao kuto kuwa na sifa
ya kufundisha kozi husika. Ref TCU reg no. 14 ibara ya 4.
4. Kukosekana kwa uwiano sawa kati ya
wafanyakazi wazawa na wageni hasa kwa ngazi za juu. Refer TCU Reg no. 14 ibara
ya 3.
5. Masomo ya pre entry ama MPP hayajatolewa
kabisa hasa ikizingatiwa masomo haya
huchukua semester mzima na kuchelewesha wanafunzi kuendelea na kozi zao husika.
6. Muda wa kuhitimu masomo uwe sawa na
vyuo vingine kama utaratibu wa elimu ya nchi unavyotambua.
7. Kusajiliwa kwa kada za sayansi ya
afya na tiba katika bodi husika(full registration).
8. Uongozi wetu haujabadilishwa akiwemo
dean of faculty of health and applied science.
9. Ada haujashuka kama utaratibu wa TCU na wizara ya elimu
ulivyoelekeza.
10. Wanafunzi wote waliosimamishwa hawajarudishwa maana walipewa kesi nyingi za
kusingiziwa na zisizoeleweka
MSIMAMO WA
WANAFUNZI:
Kutokana na matatizo tajwa hapo juu
ambayo yamekuwa na mizozo mikubwa sana hapa chuoni sisi kama umoja wa wanafunzi
wa kada za afya tuna misimamo ifuatayo.
·
Bado tunaiomba serikali ituhamishe
sehemu hii maana si salama kwetu sisi wanafunzi na haina uhakika wa kozi zake
hali inayofanya wanafunzi weng huacha masomo.
·
Hatupo tayari kurudi katika majengo
ya kampala international university mpaka matatizo yetu yapatiwe
ufumbuzi(Tuhamishwe) ili chuo hiki kimalize matatizo hayo tajwa maana ni mwaka mzima umekwisha bila sisi
kusoma masomo yaliyopo kwenye kozi za afya
MASWALI YA MSINGI KWA WIZARA HUSIKA
1.
Kwanini wizara ya elimu idahili
wanafunzi kuja kusoma kampala int. university bila kuwasiliana na wizara ya
afya na bodi husika?.
2.
Kwanini chuo kinachukua wanafunzi
wasiokuwa na vigezo kwa direct entry?
3.
Nini hatima ya waathirika wa matatizo
haya ambao wamemaliza chuo na wamekosa ajira na kwa wale wanaoendelea?
4.
Ni hatua zipi za kisheria
zinachukuliwa juu ya chuo hiki ikiwa chuo cha IMTU kilikuwa na matatizo
machache kuliko haya lakini kilifungiwa?
NB:Tamko hili limetolewa na Mwenyekiti Mteule wa Wanafunzi,
David Payovela na Katibu wake Jackson Raymond.
No comments:
Post a Comment