Rais wa Fifa, Sep Blatter aliyetangaza kujiuzulu mrithi wake atapatika February |
SHIRIKISHO la Soka Duniani, FIFA limetangaza kwamba uchaguzi mkuu wa Rais utafanyika Februari 26 mwakani.
Maamuzi haya yamefanyika leo katika kikao cha kamati ya utendaji ya Shirikisho hilo kilichofanyika mjini Zurich, Uswisi.
Sepp Blatter aliyejiuzulu siku
nne baada ya kuchaguliwa amethibitisha kuwa ataendelea kukaa madarakani
mpaka uchaguzi mkuu utapofanyika kupata mrithi wake.
Wakati huo, kundi la watu
wanaoshinikiza kufanyika kwa mageuzi wamekutana leo mjini humo
wakimuomba katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan
kuongoza mapinduzi hayo.
Kundi hilo limesema Annan ni mtu
makini ambaye anapaswa kuongoza tume ya mageuzi wakati huu Dunia
ikielekea kupata mrithi wa Sepp Blatter aliyejiuzulu Urais kutokana na
kashfa nzito ya rushwa iliyokumba FIFA.
Shirika la Ujasusi la Marekani, FBI liliwatia mbaroni Maafisa saba wa ngazi za juu wa FIFA kwa tuhuma za rushwa.
No comments:
Post a Comment