STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 10, 2015

UHONDO WA LIGI KUU BARA UMERUDI TENA

Kagera Sugar
Azam

Mbeya City

Yanga

Africans Sports

Simba
UHONDO unarudi. Ndio ule uhondo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara unatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii wakati viwanja sita vitakavyowaka moto, gumzo zikiwa mechi nne tofauti zikiwamo za wapinzani wa jadi wa mikoa ya Tanga na Shinyanga.
Mjini Shinyanga Stand United itavaana na Mwadui, huku Mkwakwani kutakuwa na vita vya Wagosi Wa Kaya dhidi ya Wana Kimanumanu.
Hata hivyo mechi zinazotolewa macho ni za Jumamosi wakati watetezi Yanga watakapokuwa ugenini kwenye dimba la Mkwakwani kuvaana na Mgambo JKT, huku watani zao Simba watakuwa jijini Dar es Salaam kupepetana na vinara, Azam FC.
Ligi Kuu ilisimama kwa muda wa mwezi mmoja na ushei kupisha maandalizi na mechi za kimataifa za timu za taifa, Taifa Stars na Kilimanjaro Stars zilizokuwa zikishiriki michuano ya kuwania fainali za Kombe la Dunia na Kombe la Chalenji.
Yanga iliyoondoka asubuhi ya leo kwenda Tanga ikiwa na kiungo mshambuliaji wake mpya kutoka Niger, Issofou Boubakar Garba, ikiwa na pengo la nahodha wake, Nadir haroub 'cannavaro' aliye majeruhi na kukiwa na hatihati ya kumtuma Donald Ngoma aliyeumia mkono juzi mazoezi, ingawa ameandamana na timu hiyo.
Yanga yenye pointi 22 itavaana na Mgambo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuitambia timu hiyo katika mechi yao ya msimu uliopita ilipoifunga mabao 2-0 siku chache tangu Maafande hao walipoitoa nishai Simba, lakini nahodha wa Mgambo, Fully Maganga ametamba kulipa kisasi.
Azam wanaoongoza msimamo ikiwa na pointi 25 itaikaribisha Simba kwenye dimba la Taifa, ikiwa na sura mpya kikosini akiwamo Haji Ugando na Novatus Lufuga waliosajiliwa katika dirisha dogo.
Pambano hilo linatarajiwa kuwa kali kutokana na upinzani wa timu hizo hasa ikikumbukwa msimu uliopita walikuwa wakiwania nafasi nyuma ya Yanga na kusababisha kutuhumiana 'kuumiza'.
Mechi nyingine za wikiendi hii ni Mtibwa Sugar kuvaana na Mbeya City ugenini, Majimaji kuialika Toto Africans na Kagera Sugar kuikaribisha Ndanda na  watani wa jadi Stand Utd na Mwadui watamaliza udhia Kambarage Shinyanga.
JUmapili kutakuwa na mechi mbili ikiwamo ya Coastal Union dhidi ya watani zao wa jadi Africans Sports, huku timu zote zikiwa katika hali mbaya katika msimamo sawa na JKT Ruvu watakaokuwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kuvaana na Prisons Mbeya.
Baada ya mechi hizo za wikiendi hii, Yanga itasalia Mkwakwani Tanga kucheza na Sports katika mechi ya kiporo siku ya Jumatano ambapo pia siku hiyo Azam itaikaribisha Mtibwa Sugar huku kiporo kingine cha Simba na Ndanda kitasubiri kuchezwa Januari Mosi mwakani.

Msimamo kamili wa ligi hiyo inayorejea tena ni huu hapa:
1. Azam                9   8   1   0   20 5  25
2. Yanga               9   7   2  0   22  5  23
3. Mtibwa Sugar    9   7   1    1   12  5  22
4. Simba               9   7  0   2   15  5  21
5. Stand Utd         10  6   1  3   11  4  19
6. Prisons             10  5  2   3   10 10 17
7. Mwadui Fc         10  4   3   3   11  10  15
8. Toto Africans     10  3   4   3   6  12  13
9. Mgambo           10  3   2   5   6   9   11
10. Majimaji          10  3   2   5   6   14  11
11. Mbeya City       10  2   3   5   8   9   9
12. Ndanda             9   1    5   3   6   8   8
13. Coastal Union  10  1    4   5   2   8   7
14.JKT Ruvu           10  1   2    7   6   16  5
15. Kagera Sugar    10 1    2   7    2   13  5
16. African Sports  9   1   0   8    1    11  3

Wafungaji:
9- Elias Maguli                      (Stand)
8- Donald Ngoma                (Yanga)
     Hamis Kiiza                      (Simba)
6-Kipre Tchetche                 (Azam)
5-Amissi Tambwe               (Yanga)
4-Fully Maganga            (Mgambo)
   Miraji Athuman                  (Toto)
   Shomary Kapombe          (Azam)
  Jeremiah Juma               (Prisons)
3-Atupele Green              (Ndanda)
   Ibrahim Ajibu                   (Simba)
   Jerry Tegete                  (Mwadui)
   John Bocco                        (Azam)
   Mohammed Mkopi       (Prisons)
   Paul Nonga                   (Mwadui)
   Raphael Alpha                (Mbeya)
   Said Bahanuzi               (Mtibwa)
   Simon Msuva                   (Yanga)
   Didier Kavumbagu          (Azam)
2-Shiva Kichuya                (Mtibwa)
   Malimi Busungu              (Yanga)
   Edward Christopher         (Toto)
   Ally Myovela                 (Prisons)
   Pastory Athanas              (Stand)
   Mohamed Ibrahim       (Mtibwa)
   Mussa Kindu               (JKT Ruvu)
   Samuel Kamuntu        (JKT Ruvu)
1- Farid Mussa                       (Azam)
   Frank Domayo                   (Azam)
   Peter Mapunda            (Majimaji)
   Rodgers Fred                 (Mtibwa)
   Paul Ngway                      (Kagera)
   Themi Felix                      (Mbeya)
   Allan Wanga                      (Azam)
   Jumanne Alfadhil           (Prisons)
   Joseph Mahundi             (Mbeya)
   David Kambole               (Mbeya)
   Justice Majabvi                (Simba)
    Vincent Barnabas          (Mtibwa)  
   Mbuyu Twite                    (Yanga)
   Stamili Mbonde           (Majimaji)
   Rashid Mandawa          (Mwadui)
   Thabani Kamusoko          (Yanga)
   Michael Aidan             (JKT Ruvu)
   Najim Magulu              (JKT Ruvu)
   Kenneth Masumbuko   (Kagera)
   Kiggy Makassy              (Ndanda)
   Salim Mbonde              (Mtibwa)
   Mudathir Yahya                (Azam)
   Hassan Materema          (Sports)
   Joseph Kimwaga             (Simba)
   Alex Kondo                   (Ndanda)
   Salim Kipanga                 (Sports)
   Fabian Gwanse             (Mwadui)
   John Kabanda        (Mbeya City)
   Juuko Murshid                (Simba)
   Ally Shomary                (Mtibwa)
   Hassan Hamis             (Majimaji)
   Ismail Mohammed       (Coastal)
   Geofrey Mlawa      (Mbeya City)
   Abuu Daud                 (Mgambo)
   Malik Ndeule               (Mwadui)
   Bakar Kigodeko          (Mwadui)
   Samir Luhaba              (Majimaji)
   Nassor Kapamba         (Coastal)
   Mohammed Hussen     (Simba)
   Ditram Nchimbi         (Majimaji)
   Seleman Kibuta          (Mtibwa)
   Deus Kaseke                  (Yanga)
   Jabir Aziz                    (Mwadui)
   Juma Abdul                    (Yanga)  

Straika wa Simba atwaa tuzo Kenya

Michael Olunga
MFUNGAJI Bora wa Kombe la Kagame, na Striaka anayemezewa mate na Simba, Michael Olunga ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) katika sherehe za tuzo hizo zilizofanyika usiku wa jana Jumatano nchini humo.
Simba imekuwa ikimfukuzia Olunga tangu alipofanya vizuri na Gor Mahia katika michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika Tanzania Julai mwaka huu na Azam kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Olunga amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 19 na kuisadia Gor Mahia kutwaa ubingwa wa KPL.
Kiungo, Khalid Aucho wa Gor Mahia pia aliyekuwa akiwaniwa na Yanga alishika nafasi ya pili katika tuzo ya Kiungo Bora wa msimu.
Kipa Boniface Oluoch ambaye naye alikuwa akinyemelewa na Simba mwanzoni mwa msimu huu alifanikiwa pia kung'ara katika tuzo hizo kwa kuwatwaa tuzo ya Kipa Bora.
Olunga hata hivyo ametajwa kuwa mbioni kutua klabu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) ya Mamelodi Sundown ambayo awali ilikuwa ikimvizia Donald Ngoma wa Yanga ila ikampotezea.

Dk Magufuli atangaza Baraza lake la Mawaziri, Nape aula

http://cdn2.yatosha.com/wp-content/uploads/2015/12/jbb1.jpg
Rais Magufuli (kati) akitangaza baraza lake la mawaziri leo pembeni yake ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixVj-oa8o8h5mtB7qrIg9WGVDM6DXh5u6ZCW-onFLhTkXs-61vgU9X7eaqUoCx8GWrXRqX9ue_A7SEYgiDS6_ax4QIF8Nqf2St4KsqRNJI5bi4jLzfOrkAVdVHMOHWcl5fOJIS4j7gkR4/s640/NAPELAANA-620x400.jpg
Waziri Mteule wa Wizara ya Habari Michezo na Wasanii, Nape Nnauye
Na Tareeq Badru
HATIMAYE Rais Dk John Magufuli ametengua kitendawili cha muda mrefu juu ya sura ya Baraza lake la Mawaziri, baada ya mchana huu kulitangaza Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli ametangaza Baraza lenye watu 19, huku mawaziri wanne wa wizara nyeti ikiwamo ya Fedha na Mipango ikikosa watu wa kuzishikilia.
Jumla ya Wizara 18 zimeundwa na Dk Magufuli, huku akitangaza kufuta semina elekezi ambayo katika Utawala wa Awamu ya Nne ilikuwa kama fasheni kufanya. Dk Magufuli alisema uamuzi huo wa kufuta semina elekezi hiyo ina lengo la kuokoa Sh Bilioni 2 ambazo zingetumika na kusema ni bora zitapelekwa kwenye Elimu kusaidia kutatua tatizo la Madawati.
Baraza hilo jipya la Awamu ya Tano ina sura mchanganyiko ikiwamo wazoefu waliokuwa katika uongozi uliopita, wengine wapya na mmoja Prof Sospter Muhongo ambaye alikuwa gumzo katika sakata ya Escrow lililoibuliwa mwishoni mwa Bunge la 10. Wizara ya Habari, Michezo na wasanii imepewa Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM Bara, Nape Nnauye.


Baraza hilo jipya la Dk Magufuli lipo hivi:

Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora: George Simbachakene  na Angella Kairuki
Naibu: Seleman Jaffo
Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira: January Makamba
Naibu: Luhaga Mpina
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu: Jenista Muhagama
Manaibu: Dk. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi: Mwigulu Nchemba
Naibu: William Ole Nasha
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano: Hajapatikana
Naibu: Inj. Edwin Ngonyani
Wizara ya Fedha na Mipango:Hajapatikana
Naibu: Ashantu Kizachi
Wizara ya Nishati na Madini: Prof. Sospter Muhongo.
Naibu: Medalled Karemaligo.
Wizara ya Katiba na Sheria: Dk. Harrison Mwakyembe
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa: Dk. Augustino Mahiga
Naibu: Dk. Susan Kolimba.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa: Dk. Hussein Mwinyi
Wizara ya Mambo ya Ndani:Charles Kitwanga.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi: William Lukuvi
Naibu: Angelina Mabula
Wizara ya Maliasili na Utalii: Hajapatikana.
Naibu: Inj. Ramol Makani
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji: Charles Mwijage.
Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi: Hajapatikana
Naibu: Inj. Stella Manyanya
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto: Ummy Mwalim
Naibu: Dk. Hamis Kigwangala
Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo: Nape Nnauye
Naibu: Anastasia Wambura.
Wizara ya Maji na Umwagiliaji: Prof. Makame Mbarawa
Naibu:Inj. Isack Kamwela