Rais Magufuli (kati) akitangaza baraza lake la mawaziri leo pembeni yake ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa |
Waziri Mteule wa Wizara ya Habari Michezo na Wasanii, Nape Nnauye |
HATIMAYE Rais Dk John Magufuli ametengua kitendawili cha muda mrefu juu ya sura ya Baraza lake la Mawaziri, baada ya mchana huu kulitangaza Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli ametangaza Baraza lenye watu 19, huku mawaziri wanne wa wizara nyeti ikiwamo ya Fedha na Mipango ikikosa watu wa kuzishikilia.
Jumla ya Wizara 18 zimeundwa na Dk Magufuli, huku akitangaza kufuta semina elekezi ambayo katika Utawala wa Awamu ya Nne ilikuwa kama fasheni kufanya. Dk Magufuli alisema uamuzi huo wa kufuta semina elekezi hiyo ina lengo la kuokoa Sh Bilioni 2 ambazo zingetumika na kusema ni bora zitapelekwa kwenye Elimu kusaidia kutatua tatizo la Madawati.
Baraza hilo jipya la Awamu ya Tano ina sura mchanganyiko ikiwamo wazoefu waliokuwa katika uongozi uliopita, wengine wapya na mmoja Prof Sospter Muhongo ambaye alikuwa gumzo katika sakata ya Escrow lililoibuliwa mwishoni mwa Bunge la 10. Wizara ya Habari, Michezo na wasanii imepewa Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM Bara, Nape Nnauye.
Baraza hilo jipya la Dk Magufuli lipo hivi:
Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora: George Simbachakene na Angella Kairuki
Naibu: Seleman Jaffo
Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira: January Makamba
Naibu: Luhaga Mpina
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu: Jenista Muhagama
Manaibu: Dk. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi: Mwigulu Nchemba
Naibu: William Ole Nasha
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano: Hajapatikana
Naibu: Inj. Edwin Ngonyani
Wizara ya Fedha na Mipango:Hajapatikana
Naibu: Ashantu Kizachi
Wizara ya Nishati na Madini: Prof. Sospter Muhongo.
Naibu: Medalled Karemaligo.
Wizara ya Katiba na Sheria: Dk. Harrison Mwakyembe
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa: Dk. Augustino Mahiga
Naibu: Dk. Susan Kolimba.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa: Dk. Hussein Mwinyi
Wizara ya Mambo ya Ndani:Charles Kitwanga.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi: William Lukuvi
Naibu: Angelina Mabula
Wizara ya Maliasili na Utalii: Hajapatikana.
Naibu: Inj. Ramol Makani
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji: Charles Mwijage.
Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi: Hajapatikana
Naibu: Inj. Stella Manyanya
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto: Ummy Mwalim
Naibu: Dk. Hamis Kigwangala
Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo: Nape Nnauye
Naibu: Anastasia Wambura.
Wizara ya Maji na Umwagiliaji: Prof. Makame Mbarawa
Naibu:Inj. Isack Kamwela
No comments:
Post a Comment