Wachezaji wa Serengeti Boys wakijifua mazoezi kujiandaa na mechi yao dhidi ya Shelisheli |
LAZIMA wapigwe! Kocha wa timu ya taifa ya Vijana ya Tanzania
U17 ‘Serengeti Boys’, Bakari Shime, amejigamba kuondoka na
ushindi dhidi ya Shelisheli katika mchezo wao utakaochezwa Uwanja wa Taifa,
jijini Dar es Salaam Jumapili hii.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Kocha Shime alisema timu yake ameiandaa vya kutosha ikiwa imepata mechi
kadhaa za kimataifa za kirafiki hali iliyomwezesha kukisuka vema kikosi hicho.
“Naamini
kwa maandalizi haya tutasonga mbele kwenye hatua inayofuata na vijana wana ari
ya kwenda Madgascar 2017 kwenye fainali za mashindano haya”, alisema Shime.
Mchezo huo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za
Kombe la Mataifa kwa Vijana U17 utachezeshwa na
waamuzi toka Ethiopia ambao ni Belay Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati na
wasaidizi wake ni Tigle Belachew na Kinfe Yilma Kinfe huku mwamuzi wa akiba
akiwa ni Lemma Nigussie na Kamishna wa
mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys iliyoingia kambini Juni 14, 2016 itarudiana na wapinzani wao Julai 2, 2016, endapo itafuzu hatua hii
itakutana na timu ya Vijana ya Afrika Kusini.
Naye nahodha wa timu hiyo, Issa Makamba amesema wapo
tayari kupambana na anaamini ushindi ni wao huku akiwataka mashabiki kuja
kuwashangilia.
No comments:
Post a Comment