Mavugo |
UHONDO unakolea. Klabu ya Simba imepata hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC)
za mastraika wake wawili wa kigeni, Laudit Mavugo na Frederic Blagnon.
ITC hizo zimetua leo Ijumaa mchana baada ya
kukamilisha uhamisho wao na sasa wanaweza kuanza majukumu yao Msimbazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopostiwa kwenye mitandao na Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele
ni kwamba ITC zimetua nchini leo mchana
kutoka katika mashirikisho ya soka ya Burundi na Ivory Coast.
Blagnon
Fredric Goue ametokea klabu ya Africa Sports ambao ni wapinzani wa jadi wa ASEC
Mimosas ya nchini Ivory Coast.
Wakati Mavugo yeye anatokea klabu ya Vital'O ya Burundi na kupatikana kwa
hati hizo kunamaliza utata wa uhamisho wa Mavugo ambaye kulitokea kwa maneno
toka kwa uongozi wa klabu ya Vital’O kuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja jambo
ambalo lilikanushwa na Mavugo.Mavugo amewakuna mashabiki wa Simba baada yab kupiga mpira mwingi kwenye mechi ya Tamasha la Simba Day dhidi ya AFC Leopards ya Kenya na ile mechi ya URA.
No comments:
Post a Comment