STRIKA
USILIKOSE
Monday, September 17, 2012
Mbio za Uchaguzi Mkuu SPUTANZA zaanza rasmi
MBIO za kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa Chama cha Umoja wa Wacheza Soka Tanzania, SPUTANZA, zimeanza rasmi kwa fomu za uchaguzi huo kuanza kutolewa jijini Dar.
Uchaguzi huo wa SPUTANZA unatarajiwa kufanyika Oktoba 20 na fomu hizo zimeanza kutolewa leo ambapo wanamichezo wanaotaka kugombea nafasi za juu watapaswa kulipia kiasi cha Sh 100,000 na zile za ujumbe kwa sh 50,000.
Katibu Msaidizi wa chama hicho, Abeid Kasabalala aliiambia MICHARAZO nafasi zitazowaniwa kwenye uchaguzi huo ni Uenyekiti, Umakamu Mwenyekiti, Ukatibu Mkuu na Msaidizi wake, Mhazini na Msaidizi wake ambao gharama za fomu ni Sh 100,000.
Kasabalala aliyewahi kutamba zamani na timu za Plisners na Mecco ya Mbeya, alisema nafasi nyingine katika uchaguzi huo ni Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na nafasi saba za Kamati ya Utendaji ambazo gharama zake ni sh. 50,000.
"Zoezi la uchukuaji na urudishaji wa fomu za uchaguzi mkuu wa SPUTANZA linaanza rasmi leo (jana) fomu zinapatikana eneo la Magomeni, " alisema.
Kasabalala alisema mwisho wa zoezi hilo la kuchukua na kurudisha fomu ni siku ya Ijumaa kabla ya zoezi la kuyapitia majina, pingamizi na usaili kufanyika takati kwa uchaguzi huo utakaoiwezesha SPUTANZA kupata viongozi wapya.
Katibu huyo alisema wakati zoezi hilo la uchaguzi wa taifa ukianza rasmi, chaguzi za vyama vya mikoa inaendelea kufanyika na kusema mikoa yote imetakiwa iwe imaliza chaguzi zao kabla ya Oktoba 10.
"SPUTANZA Taifa tumewashawaeleza vyama vyote vya mikoa iwe imeshafanya chaguzi zao kabla ya Oktoba 10 ili kuwawezesha viongozi wao kushiriki uchaguzi wa taifa utakaofanyika siku kumi baadae," alisema.
Mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment