Msanii Issa Kipemba |
Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kuwaona baadhi ya abiria ndani ya daladala wakirushiana trela la filamu hiyo kupitia simu zao za mikononi na yeye kuomba arushiwe kwa nia ya kuwa na ushahidi wa kutosha kwa kile alichokishuhudia.
Walipododoswa walipoipata 'trela' hilo ambayo filamu yake inahaririwa kwa sasa, abiria hao walidai wamerushiwa na jamaa yao.
MICHARAZO liliwasiliana na Issa Kipemba ambaye ndiye mtunzi na mmoja wa waigizaji wa filamu hiyo kutaka kujua juu ya jambo hilo, alidai hata yeye ameshangazwa na taarifa hizo akidai amekuwa akipokea simu tangu wiki iliyopita juu ya kuonekana kwa trela la filamu hiyo.
Kipemba alisema japo ni kweli alitengeneza 'trela' la filamu hiyo ya Injinia kwa ajili yake mwenyewe na kumpa mmoja wa rafiki yake aliyoiona, cha ajabu limesambaa hata kwa watu ambao hawakuwa na habari juu ya filamu hiyo.
"Kwa kweli wewe ni mtu wa 10 kama sikosei kunipigia simu kuniuliza juu ya jambo hilo, sijajua nani anayesambaza hilo trela, ingawa nililitengeneza kwa ajili yangu binafsi na nikampa mmoja wa watu wangu wa karibu japo sijui kama ndiye aliyesambaza au imevujia wapi," alisema Kipemba.
Mchekeshaji huyo aliyevuma na kundi la Kaole kabla ya kutoweka katika fani miaka nane iliyopita, alisema atachunguza ajue aliyevujisha 'trela' hilo, ili kuweza kumchukulia hatua zinazostahili kwa kuhofia isije 'akaumizwa', hata kabla filamu hiyo haijatoka.
Filamu hiyo ya 'Injinia', iliyoongozwa na Leah Richard 'Lamata' imeshirikisha wakali kama Kipemba, Jacklyne Wolper, Lumole Matovolwa na 'stelingi' Castro Dickson.
No comments:
Post a Comment