|
Mgeni
rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi
(kushoto) akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Mapinduzi, Nahodha wa Azam FC,
Himid Mao Mkami usiku wa jana Uwanja wa Amaan, Zanzibar baada ya timu hiyo
kutwaa taji hilo kwa kuifunga Tusker FC ya Kenya mabao 2-1 ndani ya
dakika 120.
|
|
Mshambuliaji
wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba akigombea mpira na beki wa Tusker FC,
Joseph Shikokoti katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya
dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. |
|
Mshambuliaji
wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba akimtoka mpira na beki wa Tusker FC,
Joseph Shikokoti katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya
dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. |
|
Mshambuliaji
wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba akikimbia na mpira dhidi ya beki wa
Tusker FC, Joseph Shikokoti katika mchezo wa fainali ya Kombe la
Mapinduzi usiku wa leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda
2-1 ndani ya dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili
mfululizo. |
|
Mwaikimba akifumua shuti |
|
Mshambuliaji
wa Azam FC, Seif Abdallah akimiliki mpira mbele ya beki wa Tusker FC,
Bright Jeremiah katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya dakika
120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. |
|
Mshambuliaji
wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba akimtoka beki wa beki wa Tusker FC,
Joseph Shikokoti katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa
jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya
dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. |
|
Shuti la bao, Mwaikimba akiwa amefumua shuti kuifungia Azam bao la ushindi |
|
Wachezaji majeruhi wa Azam, John Bocco 'Adebayor' kushoto na Abdulhalim Humud 'Gaucho' kulia wakiingia uwanjani |
|
Mpira
uko nyavuni, mkwaju wa Penalti wa Joackins Atudo umetinga kimiani
kuipatia Azam bao la kusawazisha huku kipa Samuel Odhiambo akigagaa
chini |
|
Hongera shujaa Mwaikimba, wachezaji wa Azam wakimpongeza mfungaji wa bao lao la ushindi |
|
Kikosi cha ubingwa jana |
|
Washindi wa pili Tusker FC kikosi chao cha jana |
|
Nahodha Himi Mao akiinua juu burungutu la fedha, Sh. Milioni 10 za ubingwa |
|
Mgeni
rasmi,
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto)
akimkabidhi donge nono la Sh. 300,000 mfungaji bora wa Kombe la
Mapinduzi, Jesse Were wa Tusker FC aliyemaliza na mabao matano usiku wa jana
Uwanja
wa Amaan, Zanzibar.
|
|
Binti aliyevamia uwanjani dakika ya 89 akitolewa nje na askari Polisi |
|
Mgeni rasmi,
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akimkabidhi
Kombe la ushindi wa pili wa Mapinduzi, Nahodha wa Tusker FC, Joseph Shikokoti usiku Uwanja
wa Amaan, Zanzibar.
|
|
Polisi wakimtoa nje binti aliyevamia uwanjani dakika ya 89 |
|
Azam wakisherehekea na Kombe lao |
|
Mwaikimba akifuaria na mashabiki Kombe lililotokana na juhudi zake |
|
Azam wakisherehekea na Kombe lao |
|
Brian Umony wa Azam amemuacha chini Joseph Shikokoti wa Tusker FC |
|
Umony na Shikokoti |
|
Mwaikimba aliyeruka hewani kuiga kichwa kwenye lango la Tusker kufuatia mpira wa kona |
|
Mwaikimba mawindoni |
|
|
Refa akijaribu kumzuia binti wakati anakatiza uwanjani |
Mwaikimba mbele ya Shikokoti |
Na Mahmoud Zubeiry,
Zanzibar
AZAM FC wamefanikiwa
kutetea Kombe la Mapinduzi usiku wa jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar baada ya
kuifunga Tusker FC ya Kenya mabao 2-1.
Kwa ushindi
huo, Azam wamezawadiwa Sh. Milioni 10, wakati washindi wa pili Tusker wamepata
Sh. Milioni 5.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Ramadhan Rajab Ibada ‘Kibo’ aliyesaidiwa na
Mwanahija Makame Mfumo na Mgaza Kindundi, hadi mapumziko hakuna timu
iliyofanikiwa kupata bao.
Azam ndio walioshambulia
zaidi katika kipindi hicho, lakini hawakuwa na bahati ya kufunga bao japo moja.
Gaudence Mwaikimba alipewa pasi nzuri na Brian Umony dakika ya 44, lakini shuti
lake kali lilidakwa na kipa Samuel Odhiambo.
Kipindi cha
pili, Tusker walirudi na moto mkali na kuanza kusukuma mashambulizi mfululizo
langoni mwa Azam.
Hiyo
iliwasaidia mabingwa hao wa Kenya kupata bao dakika ya 60, lililofungwa na
Jesse Were aliyeunganisha kwa shuti kali la kimo cha mbuzi pasi ya Robert
Omunok.
Hata hivyo,
bao hilo halikudumu sana, kwani Azam FC walisawazisha dakika ya 72 lililofungwa
kwa mkwaju wa penalti na beki Mkenya, Joackins Atudo baada ya beki wa Tusker,
Luke Ochieng kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Katika dakika
mbili za nyongeza baada ya kutimu kwa dakika 90 za mchezo huo, alijitokeza
binti mwenye umri kati ya 14 na 16 na kukatiza uwanjani akitokea jukwaa la Urusi.
Refa alijaribu
kumsimamisha, lakini aliendelea kukatiza Uwanja hadi nje ambako alipokewa na
askari Polisi na kutolewa nje kabisa ya Uwanja. Mtangazaji wa Uwanja wa Amaan,
Farouk Karim aliwatuliza mashabiki akisema binti huyo ametoroka hospitali ya
vichaa, Kidongo Chekundu na tayari Polisi wamemkamata na kumrejesha huko.
Hadi dakika
90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1 na ndipo zikaongezwa
dakika 30.
Gaudence
Exavery Mwaikimba aliipatia Azam bao la ushindi dakika ya pili tu tangu kuanza kwa
muda wa nyongeza baada ya kuwazidi nguvu na maarifa mabeki wa Tusker.
Kikosi cha
Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika,
Joackins Atudo, Kipre Balou, Humphrey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba, Brian
Umony/Malika Ndeule dk126 na Uhuru Suleiman/Seif Abdallah dk64.
Tusker FC;
Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Bright Jeremiah, Martin Kizza, Joseph Shikokoti,
Frederick Onyango/Mark Ochiambo dk93, Andrew Tolowa/Edwin Ombasa dk 55, Khalid
Aucho/Benson Amianda dk 80, Jesse Were/Andrew Sekayambya dk54, Ismail Dunga/Michael
Olunga dk52 na Robert Omunok.
No comments:
Post a Comment