Kikosi cha Leopard ambacho kipo nafasi za mkiani mwa Ligi Kuu ya nchini mwao kinatarajiwa kutua nchini leo baada ya kukwama kufanya hivyo jana, tarayi kwa mtanange huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Yanga iliyorejea wiki iliyopita kutoka Uturuki ilipoweka kambi ya mazoezi ya wiki mbili inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka kuona walichojifunza ughaibuni katika mechi hiyo dhidi ya Leopard.
Hata hivyo kikosi hicho kinaweza kumkosa mshambuliaji wa kimataifa kutoka Uganda, Hamis Kiiza ambaye ametajwa kuwa mgonjwa.
Mbali na Kiiza pia mchezaji Juma Abdul naye pia ataikosa mechi hiyo kwa kuwa ni mgonjwa, japo wachezaji wengine wapo tayari kuvaana na 'Chui Mweusi' huyo.
Yanga ilikuwa Uturuki kwa wiki mbili kwa kambi ya mazoezi na
ilirejea Jumapili alfajiri nchini. Katika ziara yake hiyo, ilicheza mechi tatu
za kujipima nguvu na kufungwa mbili na kutoka sare moja.
Katika mchezo wake wa kwanza, ilitoka sare ya 1-1 Ariminia
Bielefeld ya Daraja la Tatu (sawa na la nne) Ujerumani kabla ya kufungwa 2-1 na
Denizlispor FC ya Daraja la Kwanza Uturuki na baadaye 2-0 na Emmen FC ya Ligi
Daraja la Kwanza Uholanzi.
Hata hivyo rekodi ya wapinzani wao kutoka Afrika Kusini inatoa shaka kama itakuwa kipimo kizuri cha Yanga baada ya kuhimili mikiki mikiki ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment