WAGOMBEA 45 KUCHUANA UCHAGUZI MKUU WA TFF | |
Jamal Malinzi anayewania Urais TFF |
Athuman Nyamlani (kulia) anayewania Urais wa TFF |
Na Boniface Wambura
WANAMICHEZO
45 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utakaofanyika Februari 24 mwaka huu. Nafasi
zinazowaniwa ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe wa Kamati ya Utendaji
kuwakilisha kanda 13 tofauti.
Waombaji
wapya 11 waliojitokeza leo (Januari 18 mwaka huu) ni Richard Rukambura
anayeomba urais wakati kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kaliro
Samson, Jumbe Magati, Richard Rukambura, Omari Walii, Ahmed Mgoyi, John Kiteve,
Stanley Lugenge, Francis Ndulane, Riziki Majara na Hassan Othuman Hassanoo.
Mwisho wa
kuchukua fomu kwa waombaji wote ni leo (Januari 18 mwaka huu) saa 10 kamili
alasiri. Fomu pia zinaweza kuchukuliwa katika tovuti ya TFF ambayo ni
www.tff.or.tz na kurejeshwa kupitia email ya tfftz@yahoo.com Pia Kanuni za
Uchaguzi za TFF zinapatikana katika tovuti hiyo.
Orodha
kamili ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na
Richard Rukambura (Rais). Walioomba kuwania nafasi ya Makamu wa Rais ni Michael
Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia.
Kwa upande
wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na
Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus
Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai
na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari
Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora),
Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi
na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).
Athuman
Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na
Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange, Hassan Othman
Hassanoo, Riziki Majara na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala,
Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na
Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).
No comments:
Post a Comment