|
Sajuki akichapa mzigo enzi za uhai wake |
|
Sajuki na mkewe Wastara enzi za uhai wake |
|
Baba
yake Sajuki... Mzee Kilowoko akiwasiliana na ndugu na jamaa kwa simu
wakati akiwa kwenye msiba wa mwanawe, Tabata jijini Dar es Salaam jana. Familia imeamua Sajuki azikwe makaburi ya Kisutu jijini
Dar es Salaam kesho Ijumaa. |
|
Wasanii wa vichekesho, Mtanga
(kushoto) na Kiwewe (aliyejishika goti) wakiwa na waombolezaji wengine
katika msiba wa Sajuk.
|
|
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Sajuki |
|
Tutakukumbuka
milele Sajuki... msanii nyota wa filamu za Kibongo, Suzan Lewis
'Natasha' akiwa kwenye msiba wa Sajuki mapema leo kushiriki maandalizi
ya shughuli za mazishi, eneo la Tabata jijini Dar es Salaam |
|
Baadhi ya waombolezaji wa msiba wa Sajuki waliofika mapema Tabta |
|
Piga pale...! Sajuki (kulia) akiwa katika maandalizi ya filamu yake ya Vita wakati wa enzi za uhai wake. |
|
Waombolezaji wakiwa na majozni tele katika msiba wa Sajuki, Tabata jijini Dar es Salaam. |
HATIMAYE ule utata kuhusiana na mahala
pa kumzika msanii Juma Kilowoko 'Sajuki' umepatiwa jibu baada ya baba
yake kukubali kuwa azikwe jijini Dar es Salaam.
Kutokana na uamuzi huo, sasa msanii huyo aliyekuwa nyota na kipenzi cha wengi enzi za uhai wake atazikwa kesho saa 7:00 mchana baada ya swala ya Ijumaa kwenye makaburi ya Kisutu.
Awali,
baba wa msanii huyo alitaka mwanawe akazikwe kwao mkoani Songea. Hata
hivyo, baada ya kuketi na kujadili kwa kina na familia yake, akaamua
kutangaza kuwa mwanawe huyo kipenzi atazikwa jijini Dar es Salaam ili
kutoa nafasi kwa rafiki zake wengi aliokuwa akishirikiana nao katika
kazi zake za kila siku za kisanii kupata nafasi ya kushiriki mazishi
yake.
Mzee Kilowoko ametoa msimamo huo mpya leo hoo hii, ikiwa ni
muda mfupi tu baada ya kutangaza awali kuwa mwanawe atakwenda kuzikwa
Songea.
Sajuki amefariki leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili alikokuwa amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi na kupumua
kwa msaada wa mashine kabla ya kuaga dunia mishale ya saa 1:00 asubuhi.
Mashabiki wa filamu za Kibongo nchini
watamkumbuka marehemu kwa filamu zake kama 'Round', 'Shetani wa Pesa', 'Hero of the Church', 'Vita' na
'Briefcase, 'Revenge', 'Dhambi', 'Mboni Yangu', 'Two
Brothers', na'Behind the Scene'.
Sajuki alizaliwa mwaka 1986 Songea
mkoani Ruvuma, ameacha mke na mtoto mmoja.
No comments:
Post a Comment