STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 27, 2013

KAGERA SUGAR YAIAPIA YANGA LEO TAIFA

KIKOSI CHA TIMU YA KAGERA SUGAR KITAKACHOVAANA NA YANGA LEO KATIKA MECHI YA LIGI KUU

LICHA ya kubaini wanakabiliwa na pambano gumu na lisilotabirika leo mbele ya vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ya Kagera Sugar, imetangaza vita ikiapa 'Ama zao au za Yanga' leo kwenye uiwanja wa Taifa.
Kocha Mkuu ya Kagera, Abdallah 'King' Kibadeni Mputa, amenukuliwa jana akisema kuwa vijana wake leo watakuwa na kazi moja tu ya kuisimamisha Yanga uwanja wa Taifa, ili kuthibitisha kuwa hawakubahatrisha walipowafunga bao 1-0 mjini Kagera.
Kibadeni, nyota wa kimataifa wa zamani wa timu zaa Majimaji Songea, Simba na Taifa Stars, alisema wakati walipoifunga Yanga nyumbani kwao uwanja wa Kaitaba, Yanga walilalamika kwamba walionewa na pia kudai uwanja mbovu ndiyo uliowaponza kulala ugenini.
"Kwa vile tunacheza nao kwenye uwanja wa Taifa, uwanja mzuri na mbele ya mashabiki wao tumepania kuwatoa nishai ili kuwathibitishia kuwa hatukubahatisha tulipowalaza kwetu, tumepania kuibuka na ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri. Yanga wasitarajie mteremko," alisema Kibadeni.
Mkali huto ambaye rekodi yake ya kufunga 'hat trick' katika pambano la watani wa jadi wa soka nchini, Simba na Yanga mwaka 1977 haijavunjwa mpaka leo ikiwa zaidi ya miaka 30, alisema kikois chake kipo vyema ili kuibuka na ushindi kuweza kujisogeza kwenye nafasi za juu.
"TUnataka ushindi ambapo tukishinda tutalingana na Simba kwa kuwa na pointi 31, pia tuna mechi nne nyumbani ambazo tunaamini tutazifanya vizuri na hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kuchuana kuwania nafasi za juu za ligi hiyo," alisema Kibadeni.
Katika pambano lao lililopita lililochezwa Oktoiba 7, 2012, Yanga ililala bao 1-0 sawa na ilivyokuwa msimu uliopita ilipolala ugenini kwa kipigo kama hicho kabla ya Yanga kushinda nyumbani.
Hata hivyo Yanga kupitia Msemaji wake, Baraka Kizuguto, imetamba kuwa mtoto wao ni ule ule wa kutoa dozi ili kufanikisha azma yao ya kutwaa ubingwa msimu huu.
Kizuguto alisema vijana wao wana ari na kiu ya kuendeleza ushindi mbele ya Kagera kwa lengo la kuongeza pointi tatu muhimu zaa kuelekea kwenye ubingwa, pia kulipiza kisasi cha kulala ugenini bao 1-0 mbele ya wapinzani wao.
Yanga inaoongoza msimamo ikiwa na pointi 39, tatu zaidi ya Azam wanaoshika nafasi ya pili na nane dhidi ya watani zao wa jadi Simba ambazo watakuwa wakijiandaa na majukumu yao ya kuiwakilisha nchi kimataifa.
Iwapo Yanga itashinda itafikisha pointi 42 na kuzidi kuziacha mbali timu hizo zinazowafukuza kileleni, pia kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo tangu duru la pili lianze Januari 26 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment