NIGERIA BINGWA MPYA WA AFRIKA YAIZIMA BURKINA FASO
Wachezaji wa Nigeria wakishangilia Kombe lao la Mataifa ya Afrika
baada ya kuifunga Burkina Faso kwenye Fainali nchini Afrika Kusini jana.
Kocha wa Nigeria, Stephen Keshi akiwa ameshika Kombe ambalo awali alitwaa akiwa mchezaji mwaka 1994
Rais wa FIFA, Sepp Blatter wa pili kutoka kulia alikuwepo
Johannesbug jana, chini mashabiki wakiwa na bango na kuonyesha upendo
wa Waafrika kwake
Sunday Mba akipongezwa na wenzake kwa kufunga bao la ubingwa
Mchezaji wa Burkina Faso, Mady Panandetiguiri akivaana na kipa wa Nigeria, Vincent Enyeama
Mchezaji wa Nigeria, Victor Moses akipambana na ukuta Burkina
Faso, Bakary Kone (katikati), Mohamed Koffi (nyuma) na Djakaridja Kone
(kulia)
Shujaa wa Nigeria kwa mechi ya jana alikuwa ni Sunday Mba aliyefunga bao hilo pekee la ushindi dakika ya 40, baada ya kutokea purukushani kwenye lango la Burkina Faso.
Burkina Faso ambayo hiyo ndiyo fainali yake ya kwanza kucheza tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo, ilipigana kutaka kurudisha bao hilo, lakini bahati haikuwa yao na hivyo kujikuta wakijifuta machozi kwa kushika nafasi ya pili.
Nigeria ilitwaa taji la michuano hiyo mwaka 1980 na 1994 na baada ya hapo ilikuwa ikishuhudia mataifa mengine yakinyakua kabla ya mwaka huu ikiwa chini ya kocha mzawa Stephen Keshi aliyenyakua taji la mwisho mwaka 1994, kuibebesha taji hilo akiweka rekodi ya kuwa kocha wa 15 mzawa kubebea taji hilo dhidi ya 14 ya makocha wa kigeni wa nchi mbalimbali katika michuano hiyo ya Afrika.
No comments:
Post a Comment