Kiungo wa Arsenal, Mikel Arteta |
KIUNGO nyota wa Arsenal, Mikel Arteta anaamini kwamba umefika wakati wa Arsenal kuwekeza vya kutosha kuimarisha timu iwapo inahitaji kurejesha heshima yake katika soka la Ulaya.
Mchezaji huyo ametoa maoni yake hayo baada ya kuishuhudia timu yake iking'olewa kwenye michuano ya nyumbani na timu za Bradford City na Blackburn Rovers, huku ikiwa imepoteza mechi ya mkondo wa kwanza wa 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mabao 3-1 dhidi ya Bayern Munich.
Arsenal kwa miaka nane sasa haijawahi kutwaa taji lolote, hali inayompa hofu mchezaji huyo hasa akiangalia pengo lililopo baina yao na wanaoongoza Ligi Kuu ya Engalnd, Mancester United.
Arteta alisema kuwa pamoja na misingi mzuri ya kukuza vipaji vya wachezaji ndani ya Arsenal na falsafa iliyopo na wachezaji iliyonayo, lazima klabu ifanye manunuzi wa wachezaji wakali zaidi iwapo inapata mafanikio zaidi.
Alisema kusalia kwao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kunahitaji miujiza, sawa na kukata tamaa ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya England.
Hata hivyo alisema ni vema Arsenal ikaanza kujipanga kwa msimu ujao kwa kununua nyota watakaoweza kuijenga upya timu hiyo kuweza kukata kiu ya misimu karibu nane bila taji lolote.
"Tunatakwa kuwa bora na msimu ujao tuhahitaji kupata pointi nyingi zaidi kwa maana ya kutaka kushinda kila mchezo. Nadhani bodi inajua hili na tumaini letu msimu ujao watafanya kila jambo ili kufikia malengo hayo," alinukuliwa kiungo.
Kiungo alieleza pia sababu yake yua kuihama Everton na kutua Arsenal lengo likiwa ni kucheza Ligi ya Mabingwa na kwake ilikuwa na maana kubwa.
Juu ya pambano lao la kesho la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Arteta alikiri ni kazi kutokana ukweli wapinzani wao Bayern Munich kuwa wazuri msimu huu na walionyesha hivyo hata katika mechi ya mkondo wa kwanza walipoibuka na ushindi wa mabao 3-1.
No comments:
Post a Comment