Wabongo wanaokipiga Bandari-Kenya, Mohammed Banka, Thomas Maurice, David Naftari na Meshack Abel wakiwa katika pozi |
WACHEZAJI nyota wa zamani wa Simba, Yanga, Mohammed Banka, Thomas Maurice na David Naftar wameendelea kuing'arisha Bandari Kenya baada ya kuisaidia kupata ushindi wake wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Kenya kwa kuwalaza Sony Sugar mabao 3-0.
Bandari ikiwa uwanja wake wa nyumbani mjini Mombasa, ilipata ushindi huo na kufikisha jumla ya pointi 8 na kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na KCB yenye pointi 11.
Maurice alianza kuiandikia bao Bandari kwa kichwa akiiunganisha faulo iliyopigwa kiufundi na Banka kabla ya Naftari aliyewahi kung'ara Simba kufunga bao la pili na bao la mwisho lilitupiwa kambani na Eric Okoth aliyefunga pia kwa kichwa.
Bandari itashuka tena dimbani, Jumamosi kuvaana na mabingwa watetezi Tusker, huku Banka akisema kikosi chao kimejiandaa vya kutosha kuweza kuwashikisha adabu wapinzani wao hao wanaopkamata nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa imecheza mechi mbili tu.
No comments:
Post a Comment