STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 25, 2013

Simba, Azam kuvuna nini Ligi Kuu Tanzania Bara?

Kikosi Cha Kagera Sugar
KIVUMBI cha Ligi Kuu Tanzania Bara kinatarajiwa kuendelea tena keshokutwa kwa michezo miwili itakayozikutanisha timu za Azam na mabingwa watetezi Azam zitakazokuwa katika viwanja viwili tofauti kusaka pointi tatu muhimu za ligi hiyo baada ya kuwa 'likizo' kwa muda.
Simba wenyewe watakuwa ugenini mjini Kagera kuwakabili wenyeji wao Kagera Sugar katika pambano litakalochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba, wakati wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Azam watakuwa jijini Dar es Salaam kuikaribisha Prisons ya Mbeya.
Mechi zote hizo zinatarajiwa kuwa na upinzani mkali japo macho na masikio yataelekezwa zaidi Kaitaba katika pambano la Simba na Kagera Sugar kutokana na mwenendo wa mabingwa hao watetezi katika ligi hiyo.

Simba ambayo ilizinduka na kuongozwa na kamati maalum ya ushindi kurejesha matumaini kwa wana Msimbazi kwa kuikwanyua Coastal Union mabao 2-1 baada ya kupoteza mwelekeo watakuwa na kibarua kigumu Kagera kudhidhirisha kuwa hawakubahatisha kwa Wagosi wa Kaya.
Tayari kikosi hicho cha Simba kimeelezwa kimeshatua Bukoba, kuvaana na watengeneza Sukari hao walioapa kuisurubu Simba baada ya mechi yao ya awali kumalizka kwa sare ya mabao 2-2 jijini Dar.
Ushindi wowote kwa Kagera utavuruga mipango ya Simba kutetea kiti chake kinachoelekea kutua Yanga inayoongoza msimamo ikiw ana pointi 48 ambayo hata hivyo haitakuwa dimbani hiyo Jumatano.
Baadhi ya wachezaji wa Simba
Pia ushindi huo utamaanisha kwamba Kagera itaziengua Mtibwa Sugar na Coastal Union na kuikamata Simba iliyopo nafasi ya tatu kwa sasa ikiwa na pointi 34. Kagera wenyewe kwa sasa wana pointi 31 wakiwa nafasi ya sita hivyo wakishinda watafikisha idadi ya pointi 34 kama za Simba.
Katika pambano la jijini Dar, Azam itakuwa ikihitaji ushindi mbele ya maafande wa Magereza ili kuwafukizia Yanga waliowaacha nyuma kwa pointi 11, japo wapo mnbele mchezo mmoja.

Azam ina pointi 37 ikiwa imeshuka dimbani mara 19, na katika mechi yake ya mwisho kabla ya kwenda Liberia kwenye pambano lake la Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Barrack YCII waliambulia sare ya bao 1-1 na Polisi Morogoro.
Hata hivyo, Azam wasitarajie mteremko kwa Prisons wanaonolewa na kocha Jumanne Chale ambayo inapigana kuepuka janga la kushuka daraja ikiwa ipo nafasi ya 11 katika  msimamo wa ligi hiyo.
Kwa namna yoyote mechi zote hizo mbili zinaweza kubadilisha msimamo wa ligi hiyo kwa nafasi nyingine isipokuwa ile ya uongozi inayohodhiwa na Yanga yenye pointi 48.

Msimamo kamili wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa ni;




P W D L F A D Pts

1
20 15 3 2 37 12 +25 48
2
19 11 4 4 32 16 +16 37
3
19 9 7 3 28 16 +12 34
4
21 8 8 5 23 19 +4 32
5
21 8 8 5 23 19 +4 32
6
20 8 7 5 21 17 +4 31
7
19 8 5 6 21 17 +4 29
8
21 6 7 8 20 24 -4 25
9
21 7 3 11 14 21 -7 24
10 Previous rank: 11 20 6 4 10 19 32 -13 22
11 Previous rank: 10 20 4 8 8 11 17 -6 20
12
21 3 8 10 11 21 -10 17
13
21 3 8 10 17 28 -11 17
14
21 4 4 13 14 32 -18 16























































































































































































No comments:

Post a Comment