Kikosi cha Coastal Union |
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi kuu Simba |
MABINGWA wa zamani wa kandanda nchini, Coastal Union ya Tanga kesho inatarajiwa kushuka dimba la Taifa kupambana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ambayo ipo katika taharuki kubwa kufuatia baadhi ya vibopa wake kuachia ngazi ghafla kabla ya kutangazwa kamati maalum ya ushindi.
Simba na Coastal zitapambana katika pambano pekee la ligi kwa kesho, huku timu zote ziliwa zimelingana kwa pointi kila moja ikiwa na pointi 31 sawa na timu 'ndugu' za Mtibwa Sugar na Kagera Sugar na kulifanya pambano hilo la kesho kushindwa kutabirika mapema.
Mwenendo mbovu iliyonayo Simba ambayo katika mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ilinyukwa bao 1-0, itashuka keshi dimbani ikiwa na matumaini makubwa ya kurekebisha makosa baada ya kuunda kamai ya ushindi inayoongozwa na Malkia wa Nyuki, Rahma Al Kharoos.Hata hivyo kuundwa kwa kamati hiyo iliyotangazwa na Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang'are 'Mzee Kines' huenda isiwe dawa ya kutetereka kwa timu hiyo, iwapo wataingia uwanjani wakiamini ushindi bila kuifikiria Coastal yenyewe ikiwa ina shinikizo la mashabiki wake baada ya 'kuyumba' katia duru la pili.
Timu hiyo ililazimishwa suluhu na Ruvu Shooting katika mechi yao ya mwisho na kusababisha mashabiki hao kulalamika, japo blog ya klabu hiyo imemnukuu Mwenyekiti wao, Ahmed Hilal 'Aurora' akitamba kuwa kesho ni kesho katika mechi yao ya Simba.
Coastal katika duru la pili imeambulia pointi tisa tu kati ya 18 zilizotokana na mechi sita walizocheza wakipoteza moja kwa Kagera Sugar, kushinda mbili dhidi ya maafande wa Mgambo na JKT Oljoro, huku wakiambulia sare tatu mbele ya Prisons-Mbeya, Toto Afrika na Ruvu Shooting katika mechi yao iliyopita.
Hata hivyo Aurora alidai wangependa kushinda mechi hiyo licha ya kutambua ugumu wake mbele ya Simba huku akiahidi kufanya vema kwa mechi zao zitakazosalia kabla ya kufunga msimu ili kuzipiku timu wanazofukuzana nao kwenye kuwania nafasi ya tatu na nne katika ligi hiyo zikiwemo Mtibwa na Kagera.
na nyingine zilizosalia kabla ya ligi kwisha ili kuweza kuziacha mbali Mtibwa na Kagera Sugar wanaoifukuzia nafasi ya nne.
Alisema mechi hiyo ya kesho ndiyo itakayoamua timu ipi ishike nafasi ya tatu kati yao na Simba waliowazidi uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika pambano lao duru la kwanza lililochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga Oktoba 13, mwaka jana timu hizo zilishindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu ya 0-0.
Je, ni Coastal itakayotuliza munkari wa mashabiki na kuchochea kuni Msimbazi, au itatoa faraja kwa Simba? Tusubiri tuone hiyo kesho.
No comments:
Post a Comment