Na Boniface Wambura
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limetuma mapendekezo 10 ya
marekebisho ya Katiba yake kwa wanachama wake kwa njia ya waraka.
Mapendekezo
hayo yametumwa kwa kila nchi mwanachama kupitia waraka namba 1320,
ambapo wanachama kwa kupitia kwa mashirikisho yao ya mabara watapiga
kura ya ndiyo au hapa. Kwa upande wa Afrika, wanachama wa FIFA
wanatakiwa kuwasilisha kura zao kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF).
Baadhi
ya mapendekezo hayo ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuthibitishwa na
Mkutano Mkuu wa FIFA (FIFA Congress). Makamu wa Rais wa FIFA na wajumbe
wa Kamati ya Utendaji wanaochaguliwa katika mabara ambapo itabidi
wathibitishwe na FIFA Congress.
Muundo
wa Kamati ya Utendaji; nafasi moja ya vyama vya mpira wa miguu vya
Uingereza (British FAs) sasa inahamishiwa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Ulaya (UEFA). Pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya FIFA anatakiwa
kushiriki vikao vya Kamati ya Utendaji bila kuwa na haki ya kupiga kura.
Uchaguzi
wa Rais; mgombea anatakiwa kuungwa mkono na idadi ya kutosha ya vyama
wanachama kutoka katika mabara mawili tofauti. Ukomo wa uongozi;
kuanzisha vipindi vya uongozi. Ukomo wa umri; ukomo wa umri usiozidi
miaka 72 wakati wa kugombea utekelezwe.
Uwakilishi
wa kutosha kwa makundi yenye maslahi katika FIFA; makundi yenye maslahi
katika mpira wa miguu kama wachezaji wapate uwakilishi katika Kamati ya
Mpira wa Miguu. Uteuzi wa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia; uteuzi
sasa ufanywe na Mkutano Mkuu wa TFF.
No comments:
Post a Comment