JOSE MOURINHO NDIYE ANAYEVUTA MKWANJA MNENE
Jose Mourinho -- Anaongoza kwa mpunga wa mwaka baada ya kuingiza Sh. bilioni 29. |
Marcelo Lippi - Sh. bilioni 25/- |
Wenger -- Sh. bilioni 19.5 |
Ferguson - Sh. bilioni 12.6 |
Katika orodha hiyo mpya ya 'France Football', Mourinho yuko kileleni baada ya kuvuna euro milioni 14 (Sh. bilioni 29); euro milioni 12 (Sh. bilioni 25) zikitokana na mshahara na nyingine zikitokana na mikataba yake ya matangazo ya biashara.
Kama ilivyokuwa mwaka jana, kocha huyo wa Real Madrid amempiku Muitalia Carlo Ancelotti, aliyekamata nafasi ya pili kwa mara nyingine ingawa kipato chake kimeshuka kwa euro milioni 1.5 (Sh. bilioni 3) na sasa kuwa euro milioni 12 (Sh. bilioni 25) kulinganisha na mwaka uliopita.
Kocha wa klabu ya China ya Guangzhou Evergrande, Muitalia Marcelo Lippi anakamilisha orodha ya vinara akiwa na euro milioni 11 (bilioni 23), nafasi iliyotwaliwa mwaka uliopita na aliyekuwa kocha wa Barcelona, Mhispania Pep Guardiola, ambao hivi sasa yuko katika mapumziko yake ya mwaka mmoja kabla ya kuanza kuiongoza Bayern Munich msimu ujao.
Mholanzi Guus Hiddink, anayeiongoza klabu ya Ligi Kuu ya Urusi ya Anzhi Makhachkala, anakamata nafasi ya nne katika orodha hiyo akiwa na euro milioni 10.8 (Sh. bilioni 22), wakati raia wa Scotland, Kenny Dalglish anafuatia baada ya kuvuna euro milioni 10 (Sh. bilioni 21) alipokuwa Liverpool kabla ya kutimuliwa mwezi Juni.
Wanaokamilisha orodha ya makocha wanaolipwa pesa nyingi zaidi ni kocha wa Arsenal, Mfaransa Arsène Wenger (euro milioni 9.4 -- Sh. bilioni 19.5), kocha wa timu ya taifa ya Urusi, Fabio Capello (euro milioni 9.2 -- Sh. bilioni 19), Roberto Mancini wa Manchester City, Alex Ferguson wa Man U na kocha wa timu ya taifa ya China, José Antonio Camacho (euro milioni 6.1 -- Sh. bilioni 12.6).
No comments:
Post a Comment