WACHEZAJI wa timu ya soka ya taifa ya wanawake 'Twiga Stars' wamemgwaya
kocha wao mpya, Rogasian Kaijage kwa kuanza kutii masharti yake ikiwemo suala la nidhamu.
Wachezaji hao ambao walikuwa wanakata nywele kwa staili za ajabu
na uvaaji wa surulia na pensi kwa staili ya mlegezo wameonekana kubadilika
baada ya kuwa na kocha huyo mpya.
Kaijage ambaye amerithi mikoba ya Boniface Mkwasa baada ya
kubwaga manyanga mwaka jana alipoita timu hiyo alikaa nao kikao na kuwaeleza
kuwa hatapenda kuona wachezaji hao wakivaa staili ambazo zinaleta picha mbaya
kwa jamii.
“Niliwaambia mpira unahitaji uwe na adabu ili ufanikiwe
hivyo niwaambia wabadilike kuanzia muonekana hadi uwanjani na ndio maana
unawaoneka wamesuka vizuri na kubana nywele vizuri na kuvaa nguo sawasawa”,
alisema Kaijage
Mashabiki wa soka walishuhudia wachezaji wakiwa nadhifu kuanzia kwenye
mavazi hadi kichwani na wakifanya mazoezi kwa ari na kocha anapoita timu kila
mtu anakimbia kuwahi kufika siyo kutembea wala utani ambao hauna tija.
Naye meneja wa timu hiyo Furaha Francis amefurahishwa na
kitendo cha kocha kuwaeleza ukweli wachezaji kuwa nidhamu inaanzia kwenye
muonekano kwa jamii.
No comments:
Post a Comment