Chuji anayeumwa mafindofindo |
Wakali wengine kama hawa wapo fiti wakiendelea kujifua kuisubiri JKt Oljoro |
Yanga wanaoongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 49, ilianza mazoezi yake kwenye uwanja wa Mabatini, Dar es Salaam baada ya mapumziko mafupi ya sikukuu ya Pasaka.
Mbali na Chuji na Tegete ambao mmoja ni mgonjwa na mwingine majeruhi, wakali wengine hao wa Jangwani waliokosekana kwenye mazoezi hayo yanayoendelea jijini ni pamoja na kipa Said Mohammed na Mbuyu Twitte ambaye anauguliwa na mkewe.
Twitte ndiye aliyeizamisha Oljoro katika pambano la awali lililochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Wachezaji waliohudhuria mazoezi hayo yanayosimamiwa na kocha Ernst Brandts ni pamoja na makipa Ally Mustafa 'Barthez' na Yusuph Abdul, Shadrack Nsajigwa 'Fusso', Stephano Mwasika, Oscar Joshua, Juma Abdul, Godfrey Taita, Kelvin Yondani 'Vidic' na Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Wengine ni viungo; Omega Seme, Salum Telela, Nurdin Bakari, Frank Domayo, Rehani Kibingu, David Luhende na Haruna Niyonzima 'Fabrigas', Said Bahanuzi, Simon Msuva, Hamis Kiiza 'Diego', George Banda, Nizar Khalfan na Didier Kavumbagu ambao ni washambuliaji.
Vinara hao wamesaliwa na mechi tano ikiwemo hiyo ya Oljoro kabla ya kumaliza msimu wa Ligi Kuu 2012-2013.
Mechi nyingine ni dhidi ya Mgambo Shooting utakaochezwa ugenini mjini Tanga, JKT Ruvu Stars, Coastal Union na watani zao wa jadi Simba zitakazochezwa dimba la Taifa, Dar es Salaam.
Hata wawe majeruhi hao, lakini ushindi ni lazima
ReplyDelete