STRIKA
USILIKOSE
Saturday, April 13, 2013
Prisons yazidi kukimbia janga la kushuka daraja
MAAFANDE wa Prisons Mbeya wamezidi kupigana kuepa janga la kushuka daraja baada ya kuinyoa Ruvu Shooting kwa mabao 2-0 katika pambano lililochezwa jioni ya leo mjini Mbeya.
Ushindi huo ni wa pili mfululizo baada ya Jumatano iliyopita kuicharaza Mgambo JKT, ulipatikana kwenye uwanja wa Sokoine na kuifanya Prisons kuchupa kwa nafasi moja toka nafasi ya 10 haid ya 9.
Hata hivyo bado Prisons ina kibarua cha kuhakikisha wanashinda mechi zao mbili zilizosalia dhidi ya JKT Ruvu na Kagera Sugar kujihakikishia kusalia Ligi Kuu msimu ujao.
Habari kutoka Mbeya zinasema kuwa Mabingwa hao wa zamani wa Tanzania walipata ushindi huo kwa magoli ya kipindi cha pili yaliyowekwa yote kimiani na mchezaji wake aliyekuw shujaa leo, Elias Maguli.Maguli alifunga bao la kwanza kwa shuti akiunganisha pasi murua ya mchezaji mwenzake katika dakika ya 53 kabla ya kuongeza jingine dakika tano baadaye kwa mkwaju wa penati baada ya beki mmoja wa Ruvu kuunawa mpira langoni mwake.
Kwa matokleo hayop Prisons imefikisha pointi 26 na kuishuka Mgambo katika nafasi ya tisa na kukalia wao nafasi hiyo.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho kwa pambano kati ya Azam na Simba litakalochezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Msimamo wa Ligi hiyo baada ya mechi za leo jioni;
P W D L F A D PTS
1. Young Africans 22 16 4 2 40 12 +28 52
2. Azam 22 14 4 4 39 17 +22 46
3. Kagera Sugar 22 10 7 5 25 18 +7 37
4. Simba 21 9 8 4 30 19 +11 35
5. Mtibwa Sugar 23 8 9 6 26 24 +2 33
6. Coastal Union 22 8 8 6 23 20 +3 32
7. Ruvu Shooting 23 8 6 9 21 22 -1 30
8. JKT Oljoro FC 23 7 7 9 22 27 -5 28
9. Tanzania Prisons 24 6 8 10 14 21 -7 26
10.JKT Mgambo 22 7 3 12 14 22 -8 24
11.Ruvu Stars 21 6 4 11 19 34 -15 22
12. Toto Africans 24 4 10 10 22 32 -10 22
13. African Lyon 23 5 4 14 16 35 -19 19
14. Polisi Morogoro 23 3 10 10 11 21 -10 19
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment