SIMBA, AZAM HAKUNA MBABE, YANGA YAPUMUA KILELENI
Mshambuliaji
wa Simba, Mrisho Ngassa akichuana na beki wa Azam FC, John David katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilifunga mabao 2-2 (Picha na
Habari Mseto Blog)
Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa akimtoka beki wa Azam
FC, Joockins Atudo wakati wa mchezo wa Ligi Kuu
Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
jana. Timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya kuapata bao la pili.
Kiungo
wa timu ya Simba, Abdallah Seseme akiwatoka wachezaji wa Azam FC, Himid Mao
(kulia) na Salum Abubakar wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo
zimetoka sare ya mabao 2-2.
LICHA ya tambo nyingi kabla ya pambano lao timu za Simba na Azam jioni ya leo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na kuwafanya vinawa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kupumua.
Yanga mabo mashabiki wake leo walionyesha kioja kwa kuwashangilia watani zao Simba dhidi ya Azam, wanapumua kwa vile Azam inayowafukuza kwenye mbio za ubingwa imepunguza pengo la pointi moja tu na kuipa nafasi Yanga kuhitaji pointi tano tu kati ya mechi zake nne zilizosalia kutangaza ubingwa msimu huu.
Yanga yenyewe ina pointi 52 wakati Azam waliopo nafasi ya pili wana pointi 47, huku kjwa sare hiyo ya leo Simba imeendelea kusalia kwenye nafasi ya nne akiwa na pointi 36.
Ramadhani Singano 'Messi' ndiye aliyeipa Simba uongozi wa mabao katika pambano hilo lililochezeshwa na mwamuzi Oden Mbaga kwa kufunga mabao mawili katika dakika ya 10 na 14 akimalizia kazi murua iliyofanywa kwa ushirikiano wa Mrisho Ngassa na Haruna Changono.
Dakika ya 29 Kipre Tchetche aliifungia Azam bao la kwanza baada ya Khamis Mcha kuangushwa akielekea kumsalimia kipa Abel Dhaira na kumfanya afikishe bao la 15 msimu huu.
Dakika mbili baadaye kocha wa Azam, Stewart Hall alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi kutokana na maamuzi yake na hadi mapumziko matokeo yalikuwa mabo 2-1.
Kipindi cha pili Azam walionyesha uhai zaidi kwa kushambulia lango la Simba na kufanikiwa kupata bao la pili na la kusawazisha dakika ya 72 kupitia kwa Humphrey Mieno.
Kwa matokeo ya pambano hilo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kutokana na tambo zilizokuwa zikitolewa na pande zote mbili na mkasa ulioibuka baada ya mechi yao ya kwanza ambapo Simba walishinda mabao 3-1 na kupelekea Azam kusimamisha wachezaji wake wanne kwa tuhuma za rushwa, msimamo upo hivi;
P W D L F A D PTS
1. Young Africans 22 16 4 2 40 12 28 52
2. Azam 23 14 5 4 41 19 22 47
3 . Kagera Sugar 22 10 7 5 25 18 7 37
4. Simba 22 9 9 4 32 21 11 36
5. Mtibwa Sugar 23 8 9 6 26 24 2 33
6. Coastal Union 22 8 8 6 23 20 3 32
7. Ruvu Shooting 23 8 6 9 21 22 -1 30
8. JKT Oljoro FC 23 7 7 9 22 27 -5 28
9. Tanzania Prisons 24 6 8 10 14 21 -7 26
10.JKT Mgambo 22 7 3 12 14 22 -8 24
11.Ruvu Stars 21 6 4 11 19 34 -15 22
12. Toto Africans 24 4 10 10 22 32 -10 22
13. Polisi Morogoro 23 3 10 10 11 21 -10 19
14. African Lyon 23 5 4 14 16 35 -19 19
No comments:
Post a Comment