Simba |
Azam |
SIMBA na Azam jioni ya leo wanatarajiwa kushuka dimbani kumenyana katika pambano pekee la Ligi Kuu Tanzania Bara inayoelekea ukingoni huku, ambalo limetabiriwa na wengi kama vita ya kisasi baina ya timu hizo.
Timu hizo zitakutana kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kila moja ikiwa na malengo tofauti, Azam kulipa kisasi ya kipigo cha mabao 3-1 ilichopewa kwenye pambano lao la kwanza lililosababisha iwasimamishe wachezaji wake wanne kwa tuhuma za kuihujumu kupitia rushwa.
Simba wenyewe wakaikabilia Azam wakiwa na hasira za kutuhumia na rushwa sakata ambalo lilimalizwa nna Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kuibuka ikitaka kulipwa fidia ya Bilioni 1 kwa tuhuma hizo nzzito.
Pia Simba inashuka uwanja wa Taifa ikiwa inataka kulinda heshima yake katika ligi ya msimu huu kutokana nna ukweli imeshatemeshwa ubingwa na ipo hatua chachee kukosa hata nafasi ya uwakilishi wa nchi katika michuano ya Kimataifa mwakani.
Tayari kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' ametamka wazi kwamba wanashuka dimbani leo kwa lengo moja tu la kutaka kulinda heshima yao mbele ya Azam na pia kuhakikisha wanamaliza ligi wakiwa katika nafasi nzuri baada ya kutemeshwa taji.
Azam mbali na kuhitaji kulipa kisasi kwa Simba ikiamini kwamba mechi ya kwanza walifungwa kwa hila, lakini pia inasaka ushindi ili kuifukuzia Yanga kileleni ambayo jana ilitakata kwa kupata ushindi wa mabao 3-0 mbele ya maafande wa JKT Oljoro na kuzidi kujichimbia kwenye nafasi ya kwanza.
Yanga mbali na kuendelea kuongoza na kuongeza pendo la pointi dhidi yake na Azam, pia imejihakikisha nafasi ya kushiriki michuano ya Afrika mwakani mpaka sasa kati ya nafasi mbili za uwakilishi wa nchi.
Kwa kuangalia mazingira hayo, huku Azam wakijinafasi kwamba kiu yao ni kutwaa ubingwa msimu huu na kuweka rekodi, ni wazi pambano la jioni litakuwa ni patashika nguo kuchanika.
Wachezaji wanne waliohusishwa na tuhuma za rushwa baada ya pambano hilo la duru la kwanza, nahodha wa zamani Aggrey Morris, Said Morad, Erasto Nyoni na kipa Deo Munishi 'Dida' tayari wameripoti kambini katika kikosi cha timu hiyo wakielezwa wanaweza kushuka dimbani leo kuwakabili 'Mnyama'.
Hata hivyo kwa mazingira yalivyo huenda ikawa vigumu kwa wachezaji hao kucheza pambano hilo ikizingatiwa kwamba ni Simba hao hao waliowaponza hata kuingia matatani kabla ya kusafishwa na TAKUKURU.
Mashabiki wa soka watakuwa na hamu kubwa ya kuona kipi kitakachotokea katika mechi hiyo baada ya dakika 90 huku macho na masikio yakielekezwa kwa washambuliaji nyota wa Azam, Kipre Tchetche na John Bocco 'Adebayor'.
Tchetche anaangaliwa kutokana na kasi yake ya ufungaji mabao akifunga karibu kila mechi tangu arejee dimbani katika duru la pili, huku Adebayor kwa bahati yake ya kuitungia Simba kila timu hizo zinapokutana.
Bila shaka kujua nani atakayecheza ua kulia leo taifa ni suala la kusubiri kuona baada ya dakika 90 za pambano hilo la kusisimua.
No comments:
Post a Comment