Na Boniface Wambura
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Aprili
14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,855,000
kutokana na watazamaji 11,458.
Kiwnago hicho ni kikubwa kuliko pambano lililochezwa Jumamosi kati ya Yanga na JKT Oljoro ambapo mchezo huo uliingiza kiasi cha Sh Milioni 63.
Kwa pambano la jana, viingilio
katika mechi hiyo namba 155 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya
mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku
kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,198,220.34.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,925,683.45,
tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07, Kamati ya Ligi
sh. 4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,377,705.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,849,326.14.
Katika pambano la Yanga na Oljoro jumla ya Watazamaji
11,021 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya
Yanga na Oljoro JKT iliyochezwa juzi (Aprili 13 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 63,170,000.
Viingilio
katika mechi hiyo namba 156 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi
wa mabao 3-0 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000
huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,853,252.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,636,101.69.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,552,501.25,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,531,500.75, Kamati ya Ligi
sh. 4,531,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,265,750.37 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,762,250.29.
No comments:
Post a Comment