|
Baadhi ya matukio yanayoendelea Mtwara |
HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema hali ni tete mjini Mtwara, hakuna amani, mabomu ya machozi yanarindima muda
huu na huduma zote za kijamii zimefungwa hakuna usafiri, masoko, maduka
na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi kazi.
Kwa
ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na
wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi
ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.
Kufuatia
Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la
gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam ilihali Waziri wa Nishati akisoma
hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi
linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam Wananchi wa Mtwara
walicharuka!
Daraja la Mikindani limevunjwa hakuna mawasiliano Mtwara na Dar es salaam.
Baadhi ya Wananchi wamepora Silaha na wanazitumia kujibu mashambulizi ya Jeshi la Polisi (habari haijathibitishwa rasmi)
Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto.
Lodge/Hotel
(Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la
Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea
imechomwa moto.
Milio ya risasi na mabomu ndicho kinachosikika.
Nyumba kadhaa za watumishi wa Serikali zimechomwa maeneo ya Shangani.
Ni
magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo yanapata wakati mgumu
kupita kwasababu ya mawe na magogo makubwa yaliyowekwa na Wananchi.
Askari kadhaa wamekufa (habari hii haijathibitishwa rasmi)
Baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari kwakuwa wamepita jirani na gari yao.
Yadaiwa askari wengi waliokuja si wa Mtwara, wengi wametoka Masasi na Lindi.
Ving'ora vinalia hovyo. Watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia.
Vituo
vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari bali vinapiga
Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya ili
Wananchi wayapate.
Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara, mpaka sasa takriban mabomu 20 na ushee yameshapigwa.
No comments:
Post a Comment