STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, May 22, 2013

Simba, Yanga zitaanza hivi Kagame Cup 2013

http://www.gushit.com/files/bookmark_photos/542db1350bL.jpg
Hamis Kiiza 'Diego' akiwa na taji la Kagame, Yanga ilipotwaa kwa mara ya pili mwaka jana jijini Dar


MABINGWA watetezi wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), Yanga wataanza kutetea taji lao dhidi ya Express ya Uganda katika mechi ya kundi C Juni 20 kwenye Uwanja wa Elfasher saa nane mchana wakati Simba iliyopangwa kundi A la 'kifo' itashuka dimbani siku inayofuata kuivaa El Mereikh.

Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo yatakayoanza Juni 18 hadi Julai 2 mwaka huu iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), timu nyingine zinazounda kundi C pamoja na Yanga ni Vital'O ya Burundi na Ports ya Djibouti wakati kundia la kundi A la Simba linahusisha pia timu za APR ya Rwanda na Elman ya Somalia.

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa kundi B limezoa timu wenyeji zote tatu za Al Hilal, Al Nasri na Al Ahly Shandy pamoja na Tusker ya Kenya na Super Falcon kutoka Zanzibar.

Yanga ambao ni mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara watashuka tena dimbani Juni 22 mwaka huu kuikabili Ports na watakamilisha mechi za hatua ya makundi Juni 25 kwa kuvaana na Vital'O.

Wawakilishi wengine wa Bara, Simba watatupa karata yao ya pili Juni 23 kwa kuwavaa APR na watamaliza na Elman Juni 26.

Mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo itakayofanyika Juni 18 saa nane mchana itakuwa ni kati ya Tusker dhidi ya Super Falcon na saa 10:00 jioni Al Hilal itachuana na Al Nasri.

Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, alisema jana kuwa timu nane zitakazosonga mbele kucheza hatua ya robo fainali ambapo mbili kutoka makundi ya A na C, tatu kutoka kundi B na moja (best looser) itakayofanya vizuri kutoa kundi lolote.

Musonye alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na zawadi za mashindano hayo mwaka huu zitaongezeka kufuatia wadau kujitokeza kusaidia michuano hiyo.

Alisema kwamba sasa CECAFA ina jumla ya Dola za Marekani 100,000 za zawadi lakini kiwango cha fedha watakachopata mabingwa, washindi wa pili na watatu kitajulikana baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo itakayokutana kabla ya kuanza kwa mashindano hayo ya kila mwaka.

No comments:

Post a Comment