STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, June 17, 2013

Langa Kileo kuzikwa leo, wengi wamlilia

Langa Kileo enzi za uhai wake
WAKATI mwili wa msanii wa kizazi kipya, Langa Kileo, aliyefariki Juni 13 ukitarajiwa kuagwa na kuzikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam, wasanii wenzake na watu mbalimbali maarufu wametoa salamu zao za pole wakionyesha kuguswa na vifo mfululizo vya wasanii nchini.
Baadhi ya wasanii na mastaa hao kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii wamesema kifo cha Langa ni kama kutoneshwa kidonda cha msiba wa Albeert Mangweha aliyefariki Mei 28 nchini Afrika Kusini na kuzikwa Juni 6 mjini Morogoro.
Wasanii kama Hammer Q, Nikki Mbishi, Joh Makini ambaye naye alikuwa akisumbuliwa na malaria, Fina Mango, Teddy Kalonga, MwanaFA wamelezea kusikitishwa na kifo cha Langa na kumtakia mapumziko mema.
Teddy Kalonga aliandika katika ukurasa wake wa facebook akihoji inakuwaje watu wengi wanakufa wakiwa vijana wadogo katika zama hizi, huku Joh Makini akiweka bayana kwamba hatatoa kazi yake yoyote mpya ili awaomboleze wasanii wenzake waliotangulia mbele ya haki.
Fina Mango yeye alitoa pole kwa baba na mama Langa Kileo na kuwataka kuwa na uvumilivu na subira katika kipindi hiki cha msiba wa mtoto hukuywao aliyemtakia safari njema huko aendako.
Langa Kileo alifariki jioni ya Alhamisi iliyopita baada ya kuugua ghafla na kukimbizwa Muhimbili na anatarajiwa kuagwa leo saa 7 kabla ya kuzikwa baadaye kwenye makaburi ya Kinondoni, huku msiba wa Ngwair na muigizaji Taji Khamis 'Kashi' ukiwa bado haijasahaulika baada ya kufululizana.

No comments:

Post a Comment