WAKATI
Dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya ugonjwa wa Sickle
Cell mnamo Juni 19, imefahamika kuwa Tanzania ina madaktari wanne tu wa kutibu ugonjwa huo kitu alichodai huenda ndiyo sababu ya ongezeko la ugonjwa huo ambapo Tanzania inashika nafasi nne duniani kwa sasa.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Motion Arts Production (MAP), Honeymoon
Aljabri, ndiye aliyefichua hato juzi alipokuwa akieleza maandalizi yao ya kufanya maonyesho ya michoro itakayoonyesha rasilimali za nchi Tanzania pamoja na kujadiliana na wadau mbalimbali juu ya
ugonjwa huo.
Maonyesho hayo ya uchoraji yanaanza leo katika Jumba la Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam.
Aljabir alisema
takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya nne duniani kwa kuwa na wagonjwa
wengi wa Sickle Cell hivyo ni wakati muafaka kwa kila mtu kujitokeza kusaidia
kukabiliana na ugonjwa huo.
Alisema ni kitu cha ajabu kwamba pamoja na ugonjwa huo kuwa tishio lakini nchi ina madaktari wanne tu ambao alidai hawatoshi kukabiliana na ugonjwa huo.
“Siku ya Jumatano ni siku ya Sickle Cell Duniani, tumeona ni vyema kuwaeleza Watanzania wakatambua
kuwa nchi yao ina waathirika wengi wa ugonjwa huo ikishika nafasi ya nne duniani, lakini ikiwa na idadi ndogo ya madaktari kwa sasa wakiwa ni wanne tu kwa nchi nzima, idadi ambayo haitoshi," alisema.
Mwasisi
huyo wa MAP pamoja na kutumia maonyesho hayo pia
tunatarajia kufanya matembezi ya kilometa tano mwezi Septemba ambao ni mwezi
uliopangwa duniani kote kuwa mwezi wa kupata elimu kuhusu ugonjwa huu wa Sickle Cell.
Aljabri alisema katika matembezi hayo tunatarajia
kuchangia damu pamoja na shughuli nyingine mbalimbali za kijamii ili kuweza
kuwasaidia waathirika wa ugonjwa huo hapa nchini,pamoja na juhudi zetu hizo
malengo ya kudumu ni kufungua kituo cha
taarifa ambacho kitasaidia watu wenye Sicle Cell kupata taarifa juu ya maradhi hayo na hupatikanaji wa huduma zake.
Mkurugenzi
huyo alisema mwaka huu wataendesha kampeni hiyo katika mkoa wa Dar es
Salaam pekee ila matarajio yao ni kuhakikisha kuwa kwa miaka ijayo wanafika
kwenye mikoa yote nchini.
No comments:
Post a Comment