Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, John Tendwa |
Na Suleiman Msuya
MSAJILI wa
Vyama vya Siasa nchini John Tendwa amesema ili kuhakikisha kuwa amani
inaendelea kudumu ni muhimu kuwepo kwa uvumilivu na kuheshimiana kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kauli hiyo ameitoa leo Ofisini kwake Jijini Dar es
Salaam ikiwa ni siku chache baada ya kutokea kwa mlifuko wa bomu kwenye mkutano
wa kampeni ya udiwani uliokuwa unaendeshwa na CHADEMA katika viwanja vya Soweto
mjini Arusha.
Tendwa alisema kwa muda sasa kumekuwepo kwa msuguano
mkubwa baina ya vyama hivyo viwili jambo ambalo linaonyesha dalili za
kuhatarisha amani ya nchi na wananchi kwa ujumla.
Msajili huyo alisema vyama hivyo vinaonyesha
kukosa uvumilivu na kuheshimiana kwani
kwa kipindi hiki kifupi cha kampeni za udiwani viomekuwa na fujo ambazo kila
mmoja anamshutumu mwenzake jambo ambalo sio nzuri katika nchi.
Alisema kutokana na tukio hilo viongozi wao
wameibuka na kushutumiana ambapo Katibu Uenezi
wa CCM Nape Mnauye alisikika akiwashutumu CHADEMA kuhusikana wakati Mwenyekiti
wa CHADEMA Freeman Mbowe akisema CCM na Jeshi la Polisi wanahusika.
“Inasikitisha sana kuona watu wanakufa alafu watu
wanajitokeza na kuanza kushutumiana kuwa huyu ndiye anahusika mimi nomba
wapeleke ushahidi Jeshi la Polisi ili kuweza kusaidia upelelezi,” alisema.
Tendwa alisema katika kuhakikisha kuwa vyama hivyo
vinaendelea kuheshimiana na kuvumiliana anatarajia kuita kikao ambacho
kitashirkisha ofisi yake, jeshi la polisi na vyama hivyo kwani wanapoelekea ni
pabaya.
Alisema iwapo uchaguzi wa Udiwani hali inakuwa hivyo
je itakuwakuaje katika uchaguzi wa Serikali za Mitaaa na uchaguzi mkuu watu
watarajie nini kwani ni ishara mbaya kwa Taifa ambalo linasifika kwa amani.
Aidha Msajili huyo alipotakiwa kuelezea juu ya ofisi
yake kuvifuta vyama hivyo viwili vya CCM na CHADEMA alisema ofisi yake ina
mamlaka hayo ila hiyo ni hatua ya mwisho kuchukuliwa iwapo itabidi.
Tendwa alisema uamuzi wa kuvifuta vyama hivyo
unaweza kuwa na athari kubwa kwani utahitaji gharama kubwa za kufanyika
uchaguzi jambo ambalo sio la kukimbilia.
Alisema ofisi yake inahitaji kukutana na vyama
hivyo kwani ndio njia sahihi ya kufikia
muafaka kwa maslahi ya vyama hivyo na wananchi kwa ujumla.
“Ni lazima jamii itakatumbua kuwa maamuzi haya
yanahusi CCM ambayo ipo madarakani ambapo matokeo yake ni kuvunja Serikali na
kwa CHADEMA ni kuwaondoa wabunge wake hivyo uchaguzi kufanyika tena,” alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya
Siasa nchini Peter Mziray amevitaka vyama hivyo kutambua kuwa nchi hii iwapo
itaingia vitani wao ndio wahusika wakubwa.
Alisema Baraza hilo linatajia kukutana kwa pamoja
likishirikisha vyama vyote vya siasa ambapo watatoka na azimio juu ya hali
ilivyo hivi sasa kwani inaonyesha dalili za kupotea kwa amani.
Mziray ambaye ni Rais Mtendaji wa Chama cha African
Progressive Party Tanzania (APPT Maendeleo alisema hali inayotoke kwa sasa
jeshi la Polisi na vyombo vyote vya usalama vinapaswa kushutumiwa kwani
vionyesha kutofanya kazi vizuri.
Mwenyekiti huyo alisema hali hiyo inasikitisha sana
kutokana na ukweli kuwa watu wasio na hatia kupoteza maisha jambo ambalo
halikubaliki.
“Kwa kweli vyama hivi viwili vimekuwa na matukio
mbalimbali ambayo kwa muono wangu nadhani vinahitajika kubadilika kwani hali
sio shwari ila vyombo vya usalama pia vina mapungufu yao,” alisema
No comments:
Post a Comment