RAIA wawili wa kigeni kutoka katika nchi ya Uingereza ambao wanafanya kazi ya
kujitolea katika upande wa ualimu wamemwagiwa tindi kali mjini Zanzibar
jana jioni katika mitaa ya Shangani Mji Mkongwe
visiwani Zanzibar.
Habari kutoka katika chanzo chetu cha habari kinasema Jeshi la
Polisi Zanzibar limeanza msako na kuwatafuta watu waliofanya kitendo
hicho dhidi ya walimu hao wa kike waliofika Zanzibar kwa kujitolea kufundisha
walitambulika kwa majina ya Kate Gee (18) na Kirsiwer Trup (18) na walikuwa na wiki mbili tu.
Walimu hao waliokutwa na janga hilo walikuwa wanafanya kazi katika shule moja ya msingi
inayojulikana kama Mtakatifu Monika iliyopo chini ya kanisa la Aglicana.
habari tulizozipata hivi punde Raia hao hivi sasa wamehamishiwa katika
Hospitali ya Aghakani jijini Dar es salaam kwa matibabu zaid tutazidi
kuwaleta habari zaidi.
Tukio hilo limetokea wakati hakuna taarifa zozote za matukio ya nyuma ya kumwagiwa watu tindikali visiwani humo akiwamo Katibu wa Mufti visiwani humo na yale yanayotokea Tanzania Bara maeno ya Dar na Arusha hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment