[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
WILAYA YA KYELA - AJALI
YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 07.08.2013 MAJIRA
YA SAA 08:30 HRS HUKO KATIKA ENEO
LA KALUMBULU WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. GARI
T.932 BUF AINA YA T/IPSUM
IKIENDESHWA NA KAIMU S/O HENDE, MIAKA 33, MBONDEI, MKULIMA MKAZI WA KYELA-KATI ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO HAWA
D/O GIBSON,MIAKA 6,MSAFWA,MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA S/MSINGI MBUGANI MKAZI KALUMBULU NA KUSABABISHA KIFO
CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA. CHANZO NI MWENDO KASI, DEREVA
AMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by:
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
No comments:
Post a Comment