Na Boniface Wambura
MICHUANO
ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa
katika makundi matatu msimu huu (2013/2014) itaanza kutimua vumbi
Septemba 14 mwaka huu.
Kila
timu itakayoongoza kundi lake katika ligi itakayochezwa kwa mikondo
miwili (nyumbani na ugenini) ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015.
Mechi
za ufunguzi kwa kundi A zitakuwa kati ya Tessema vs Green Warriors
(Uwanja wa Karume, Dar es Salaam) wakati Septemba 15 mwaka huu ni
Transit Camp vs Polisi Dar (Uwanja wa Mabatini, Pwani), Ndanda vs
Friends Rangers (Uwanja wa Nangwanda, Mtwara) wakati Villa Squad vs
African Lyon itachezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi
B ni Burkina Faso vs Polisi Moro (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Mkamba
Rangers vs Lipuli (Uwanja wa CCM Mkamba, Morogoro), Majimaji vs Mlale
JKT (Uwanja wa Majimaji, Songea) wakati Septemba 15 mwaka huu Kimondo SC
vs Kurugenzi (Uwanja wa Sokoine, Mbeya).
Mechi
za ufunguzi kundi C ni Polisi Mara vs Polisi Dodoma (Uwanja wa Karume,
Musoma), Kanembwa JKT vs Polisi Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika,
Kigoma), Stand United vs Mwadui (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), na
Pamba vs Toto Africans (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza).
Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Oktoba 26 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Machi 22 mwakani.
No comments:
Post a Comment