Wakili Nassor Jumaa |
WAKILI Nassor
Jumaa anayesimamia Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini,
Sheikh Ponda Issa Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya
kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, leo hii majira ya saa 7 mchana nje ya viwanja vya Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam amesema kuwa amesikitishwa na hatua
ya vyombo vya dola kumuondoa Sheikh Ponda aliyekuwa amelazwa katika wodi
ya Kitengo cha Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya
Fahamu (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha kumhamishia katika
gereza la Segerea.
Wakili Jumaa alisema amesikitisha na kitendo hicho kwani muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumaliza kumsomea Sheikh Ponda shitaka linalomkabili, Hakimu Hellen Riwa alitoa amri kuwa Sheikh Ponda aendelee kukaa chini ya ulinzi.
Jumaa akasema ameshangazwa kuona leo, wanausalama wamemtoa Sheikh Ponda wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika: “Kwa kweli kitendo hicho kime nisikitisha na kunishitua sana… ila tunatafakari ni hatua gani za kisheria tutazichukua huko siku za usoni,”alisema Jumaa.

(via Habari Mseto)
No comments:
Post a Comment