STRIKA
USILIKOSE
Saturday, September 28, 2013
Chelsea chupuchupu, Torres alimwa kadi nyekundu
BAO la nahodha John Terry, liliisaidia Chalsea kuepuka kipigo cha ugenini dhidi ya wenyeji wao, Tottenham Hotspur katika mfululizo ya Ligi Kuu ya England (EPL) mechi iliyoisha hivi punde.
Vijana wa kocha Jose Mourinho walijikuta wakishutukizwa kwa bao la mapema lililofungwa na Gylfi Sigurdsson katika dakika ya 19 na kushuhudiwa wenyeji wakitawala sehemu kubwa ya kipindi hicho.
Hata hivyo mabadiliko yaliyofanywa katika kipindi cha pili kwa kuingizwa dimbani kwa Juan Mata kuliifanya Chelsea kutakata na kushambulia lanmgo la Spurs kwa muda mrefu ikifanya kosa kosa za hapa na pale kabla ya terry kufunga bao dakika ya 65 kwa kasi kubwa iliyofanywa na Mata.
Hata hivyo makali ya Chelsea yalipunguzwa baada ya mshambuliaji wao nyota, Fernando Torres kutolewa nje ya uwanja baada ya kuonyesha kadi ya pili ya njano dakika 10 kabla ya kumalizika kwa pambano hilo.
Kabla ya hapo 'El Nino' alishaonyeshwa kadi ya njano dakika sita baada ya kuanza kwa kipindi cha pili na kuifanya Chelsea kucheza pungufu, japo waligangamala la kumaliza mchezo huo kwa sare ya 1-1 na kuifanya ifikishe pointi 11 na kuendelea kusalia nafasi ya tatu nyuma ya Arsenal yenye pointi 12 na vinara Tottenham ambao huenda wakaongoza kwa muda kwa sababu timu nyingine zipo dimbani kwa sasa japo Arsenal wenyewe watajitupa uwanjani baadaye na kama itashinda itarejea kileleni mwa msimamo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment