Mwandishi wa kampuni ya IPPMEDIA mkoa
wa Morogoro Devotha Minja akiwa mwenye huzuni huku akiwa amemkumbatia
Hamida Shariff wa gazeti la Mwananchi Morogoro jana wakati wa kuaga
mwili wa bosi wake.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera
kushoto akimpa pole baba wa Venance George, Mzee George Mhakingilwa
wakati wa misa ya kuaga mwili wa marehemu Venance, Kulia ni Mke wa
Marehemu Sauda Mgombelwa.Bendera akifafanua jambo huku George Mhangilwa (katikati) na Boninvetura Mtalimbo kulia wakisikiza jambo muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kusafirisha mwili wa marehemu Venance George kwenda kijiji cha Bukoti Geita kwa ajili ya mazishi.
Mtoto wa kiume wa Venance George, Erasto akiwa amekaa katika gari hilo.
kutoka kushoto mstari wa nyuma, Lilian
Justice (Majira) Amina Saidi (Star Tv) na Merina Robert (Mtanzania na
Clouds Fm) kila mmoja akiwa ameweka pozi la majonzi wakati wa tukio
hilo.
Mwandishi wa Tanzania Daima, Joseph
Malembeka kulia akisaidiana na mwenzake kumpa msaada mwanamke ambaye
aliishiwa nguvu wakati wa tukio la kuaga.
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU
VENANCE GEORGE.
Marehemu Venance George
Mhangilwa alizaliwa mnamo 8/12/1973 Bukoti wilaya ya Geita.
ELIMU:
-Marehemu alisoma katika shule
ya msingi Bugogo kuanzia mwaka 1981 mpaka mwaka 1987 alipohitimu elimu yake ya
msingi.
-Mnamo mwaka 1988 alianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Forest Hill iliyopo Morogoro na kuhitimu kidato cha sita mnamo mwaka 1994.
-Mnamo mwaka 1988 alianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Forest Hill iliyopo Morogoro na kuhitimu kidato cha sita mnamo mwaka 1994.
-Mwaka 1995 alijiunga katika
chuo cha uandishi wa habari na kuhitimu mwaka 1996.
AJIRA:
Marehemu alianza kazi ya uandishi
wa habari katika kampuni ya,
-Uhuru Publication Limited, 1996-1998.
-Kuna Entarprises Company
Limited, 1998-1999.
-Village Travel And Transport
Project (VTTP), 2001-2003.
-Swiss-Contact Tanzania
Limited, 2001-2003
-Mwananchi Communication
Limited, 2003 mpaka mauti yalipomkuta.
Pia alijiendeleza kimasomo
katika chuo kikuu huria cha Tanzania
ambapo alitakiwa kuhitimu shahada yake ya mawasiliano ya umma mwezi wa 12 mwaka
huu 2013.
MWISHO:
-Marehemu alikuwa akisumbuliwa
na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu na kifua hali iliyopelekea kwenda kulazwa
katika hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Dar es salaam na kupata nafuu,
Baada ya kurudi nyumbani hali ilbadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa
katika hospitali ya Holly Cross Mission iliyopo mkoani Morogoro na baadaYe
kuhamishiwa katika hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro.
Marehemu alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani , baada ya siku kadhaa hali ilibadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro hadi umauti ulipomkuta mnamo tarehe 26/09/2013 saa 9:15.
Marehemu alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani , baada ya siku kadhaa hali ilibadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro hadi umauti ulipomkuta mnamo tarehe 26/09/2013 saa 9:15.
-Marehemu ameacha mjane na
watoto wawili wa kike na wa kiume.
SHUKRANI:
-Tunatoa
shukrani zetu za dhati
kwa wale wote waliokuwa pamoja na sisi tangu marehemu alipoanza kuugua
mpaka
leo hii , shukrani ziwafikie wafanyakazi wenzake, ndugu, jamaa na
marafiki wa karibu. Maelezo haya kwa mujibu wa Mratibu wa mazishia,
Bonveture Mtalimbo.
Source:Juma Mtanda
No comments:
Post a Comment