Mwamuzi Sako Mtilya akimnyanyua mkono juu bondia Francis Miyeyusho baada ya kumshinda kwa pointi mpinzani wake Sadiki Momba wakati wa mpambano wao |
Bondia Mussa Sunga kushoto akipambana na Fadhili Awadh wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili. Awadh alishinda kwa Point |
Baadhi ya raia wa kigeni kutoka china waliokuja kumsapoti bondia Mussa Sunga wakiwa katika picha ya pamoja na bondia huyo |
DVD KALI ZA MCHEZO WA NGUMI ZINAZOSAMBAZWA NA KOCHA SUPER D |
Mashabiki wa mchezo wa masumbwi |
BINGWA wa Kimataifa wa Ngumi za Kulipwa anayetambuliwa na IBO, Francis Miyeyusho ameendeleza rekodi yake ya kuwachakaza wapinzani wake baada ya mwishoni mwa wiki kumshinda kwa pointi Sadick Momba.
Miyeyusho alipata ushindi huo siku ya Jumapili katika pambano lisilo la ubingwa lililochezwa kwenye ukumbi wa Friends Corner, Manzese jijini Dar es Salaam.
Miyeyusho aliyemchakaza hivi karibuni Mzambia Fidelis Lupupa, alionyesha tangu mwanzoni mwa mchezo huo dhamira yake ya kuibuka ushindi, licha ya Momba kuonyesha upinzani mkubwa.
Wakiviziana na kudonoana kwa zamu, mabondia hao walijikuta wakimaliza pambano hilo la uzito wa bantam bila mashabiki kutabiri mapema nani mshindi kutokana na waliovyoonyesha upinzani katika mchezo huo.
Hata hivyo baada ya kumalizika kwa mchezo na majaji kutoa matokeo yao, mwamuzi Sako Mtilya alimtangaza Miyeyusho kuwa ndiye mshindi na kufanya mashabiki waliofurika kwenye ukumbi huo kumshangilia bondia huyo.
Huo ni ushindi wa 12 mfululizo kwa Miyeyusho ndani ya ardhi ya Tanzania tangu Aprili 2009 akiwapiga mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo katika kipindi hicho, bondia huyo mwenye rekodi ya kucheza mapambano 47 na kushinda 36 akipoteza 10 na kuambulia sare mbili alishatoka nje ya nchi mara tatu na mara zote kudundwa na wapinzani wake kwa KO.
Katika pambano jingine la utangulizi Fadhili Awadh alimshinda kwa pointi Mussa Sunga katiika pambano lililokuwa limekaa ufundi.
No comments:
Post a Comment