Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred |
MWAKILISHI
wa Tanzania katika shindano la dunia (Miss World), Brigitte Alfred,
amefanya kweli baada ya kufanikiwa kutwaa nafasi ya tatu katika shindano
dogo la Beauty with a Purpose.
Mrembo huyo, anatarajiwa kupanda jukwaani leo huko Bali, Indonesia kuwania taji la Miss World.
Taji
la Beauty with a Purpose limetwaliwa na Ishani Shrestha wa Nepal na
kilichomfanya Brigitte ashike nafasi hiyo ni kutokana na video
aliyoiwasilisha kuhusu kazi alizofanya kwa jamii hapa nchini.
Video aliyoiwasilisha Brigitte ilionyesha kazi ya jamii aliyoifanya kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi.
Nafasi
ya pili ilichukuliwa Erin Holland wa Australia, huku lile la ‘Top
Model’ likitwaliwa na Megan Young wa Ufilipino, Jacqueline Steenbeek wa
Uholanzi akatwaa la michezo, Sancler Frantz wa Brazil akachukua la
‘Beach Fashion’, Vania Larissa wa Indonesia alitwaa la Miss World Talent
na Navneet Dhillon wa India akatwaa la Multimedia.
Washindi
watano katika mashindano hayo madogo wana uhakika wa kuingia hatua
inayofuata, huku Brigitte kwa nafasi hiyo ikiwa imemsaidia kwa kiwango
kikubwa kujiamini kwa kusonga mbele.
Brigitte
anashiriki fainali leo, huku akiwa na kazi kubwa ya kuhakikisha
anafuata nyayo za Nancy Sumari aliyefanikiwa kutwaa taji la Afrika
katika mashindano ya Miss World ya mwaka 2005.
Akizungumza
kutoka Indonesia, Brigitte alisema, wengi walifurahi kazi yake
aliyopeleka ambayo ilionyesha pia kwa kiasi kikubwa jinsi watu wenye
ulemavu wa ngozi wanavyohitaji msaada, hasa kutokana na kuwindwa na
baadhi ya watu.
“Waliipenda
kazi yangu, lakini kwa shindano la kesho (leo) nina uhakika mkubwa wa
kufanya vizuri, kwani vigezo vyote ninavyo na nimejiandaa kwa muda mrefu
mno.
“Niseme
wazi nimejiandaa kwa muda mrefu mno na nashukuru wote walionisaidia kwa
njia moja au nyingine na hii inanipa moyo wa kufanya vizuri zaidi,”
alisema.
Wakati
akimuaga Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella
Mukangara, alimtaka ahakikishe anaipeperusha vizuri bendera ya Tanzania
na kufanya vyema katika mashindano hayo.
“Fahamu
fika kwamba unakwenda Indonesia kama Miss Tanzania na si Brigitte,
hivyo unatuwakilisha Watanzania wote, sisi tuko nyuma yako unachotakiwa
ni kujiamini tu na utafanikiwa.”
Mrembo
huyo alifanikiwa kulitwaa taji la Redd’s Miss Tanzania mwishoni mwa
mwaka jana, akitokea kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni.
Taji
la Miss World linashikiliwa na mrembo Wenxia Yu kutoka China, ambaye
tayari alikuwa Indonesia kwa ajili ya kulivua taji hilo.
No comments:
Post a Comment