Ticotico (kushoto) katika moja ya mechi zao za maveterani |
WAKALI wa soka la maveterani jijini Dar es Salaam, Golden Bush Veterani kesho asubuhi inatarajiwa kuvaana na Pugu Veterani katika pambano la kukata na shoka la kirafiki litakalochezwa kwenye uwanja wa Kinesi, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya uongozi wa Golden Bush inayoundwa na wakali za zamani wa Simba na Yanga, mechi hiyo ni ya kumaliza mzizi wa fitina baada ya tambo za muda mrefu, huku wakali hao wa soka la jiji wakiwatisha Pugu kwamba wajiandae kupokea kipigo kikali hiyo kesho.
Taarifa ya Golden Bush kupitia Msemaji na mlezi wa klabu hiyo, Onesmo Waziri 'Ticotico' inasomeka hivi:
Wadau,
Kutokana
na vipigo vya mfululizo kutoka kwa wapinzani wetu wakiwepo Pugu
Veterans, na tambo nyingi kutoka kwa wapinzani wetu hapa jijini, Golden
bush tumelazimika kuomba mechi ya kirafiki ya marudiano na Pugu
Veterans, game itapigwa uwanja wa Kinesi maarufu kama St James Park siku
ya jumapili asubuhi. Kwakutambua umuhimu ya game hii, uongozi wetu
umeitisha kikao cha dharula kesho baada ya mazoezi asubuhi ili kuweka
mikakati kabambe ya kurudisha heshima ya timu yetu ambayo mpaka sasa
inatambulika kama mabingwa wa jiji la Dar es Salaam. Timu yetu
imekamilika kabisa hakuna majeruhi hakuna mgonjwa hakuna mgogoro, uwanja
uko sawa kamati ya ufundi inamaalizia kazi yake kwa kushirikiana na
Walimu wetu. Tumejiwekea lengo la kufunga magoli mengi iwezekanavyo ili
kuvunja rekodi ya kufunga magoli.
Aidha
ningependa kutoa taarifa kwamba timu yetu imeimarika zaidi mara baada
ya Juma Kaseja, Said Swedi ,Mwarami Mohamed na Shadrack Nsajigwa
kurejea kwenye timu yetu. karibuni mje muone soka la hali ya juu sana
huku likihanikizwa na ufundi wa vijana wa zamani chini ya kocha wetu
Madaraka Selemani “Mzee wa kiminyio”
Baada ya game ya jumapili, timu itakuwa kwenye maandalizi ya mwisho kabisa kwenda kucheza mechi za kirafiki visiwani Zanzibar.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Onesmo Waziri “Ticotico” Mchezaji Mwandamizi
No comments:
Post a Comment