Simba walioshinda jijini Dar |
Yanga iliyotakata mjini Bukoba kwa kuilaza Kagera Sugar |
Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 katika pambano kali lililochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam dhidi ya maafande wa Magereza, Prisons-Mbeya na kufikisha jumla ya pointi 18.
Kiti cha Simba kilikuwa hatarini siku ya leo iwapo kama ingeteleza na matokeo iliyopata watani zao wa jadi mjini Bukoba, baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao Kagera Sugar.
Mkude alifunga bao hilo katika dakika ya 61 na kuiokoa timu yake kugawana pointi na Prisons iliyoonyesha upinzani mkubwa katika pambano hilo.
Bao hilo ambalo ni la tatu kwa Mkude katika orodha ya wafungaji mabao, lilikuwa likusubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Simba ambao dakika 45 za kwanza walikuwa wanyonge na hasa walipokuwa wakipata matokeo ya pambano la mjini Bukoba.
Kwa ushindi huo Simba imesalia kileleni na kufuatiwa na Yanga ambao walipata mabao yake kupitia kwa Mrisho Ngassa aliyefunga kwa kichwa dakika moja tu baada ya pambano hilo kuanza bao lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha kilianza kwa wenyeji Kagera Sugar kusawazisha bao dakika mbili baada ya kuanza kwa kipindi hicho, lakini Yanga ilidhihirisha kuwa ilipania kuilipa kisasi na kufuta unyonge wake mbele ya Kagera kila wanapokutana Kaitaba kwa kuongeza bao la pili.
Mganda Hamis Kiiza 'Diego' alifunga bao hilo katika dakika ya 57, goli linalomfanya afikishe jumla ya mabao matatu mpaka sasa katika ligi ya msimu huu, ikiwa ni wiki moja kabla ya timu yake ya Yanga kukabiliana na Simba katika pambano la watani wa jadi litakalochezwa Okt. 20.
Ushindi huo wa Yanga umeifanya mabingwa watetezi hao kufikisha pointi 15, tatu nyuma ya Simba na iwapo itafanikiwa kushinda katika mechi yao ya Jumapili ijayo, huenda vijana hao wa Jangwani wakakikalia kiti cha uongozi baada ya kuenguliwa walipoyumba katika ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment