Na Boniface Wambura
MRADI
wa Football for Hope kusaidia watoto na wasiojiweza kupitia mpira wa
miguu uliofadhiliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
mkoani Iringa utafunguliwa rasmi Oktoba 13 mwaka huu.
FIFA
hutoa mradi huo kwa baadhi ya nchi kwa kuzingatia mambo mbalimbali
ikiwemo utawala bora, lakini kwa kupitia taasisi zisizo za kiserikali
(NGOs) ambapo kwa Tanzania umepatikana kupitia taasisi ya Iringa
Development of Youth, Disabled and Child Care (IDYDCC).
Rais
wa TFF, Leodegar Tenga ameishukuru FIFA kwa msaada huo, kwani ni mkubwa
na kuongeza kuwa ni matumaini yake utatumika kwa lengo lililopangwa.
Amesema
mradi huo wa FIFA ambao ni wa kusaidia watoto kielimu na wasiojiweza
kwa kupitia mpira wa miguu haukupita moja kwa moja TFF ni mzuri kwani
moja ya mambo uliofanikisha ni kuwepo jengo na sehemu ya watoto kucheza.
Ni
wastani wa nchi kumi tu duniani kwa mwaka zinapata mradi huo kutoka
FIFA, jambo ambalo Rais Tenga amesema linachangiwa pia na uhusiano na
ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na shirikisho hilo.
No comments:
Post a Comment