PAMBANO la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) iliyochezwa jana (Oktoba 6 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Yanga na Mtibwa Sugar limeingiza
sh. 97,557,000.
Watazamaji
waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 46 lililochezeshwa na
Isihaka Shirikisho kutoka Tanga walikuwa 17,313. Yanga ilishinda mabao
2-0.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 23,453,748.95 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,881,576.27.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,925,635.06,
gharama ya kuchapa tiketi ni sh. 3,171,190 wakati gharama za mchezo ni
sh. 7,155,381.04.
Kamati
ya Ligi sh. 7,155,381.04, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF)
sh. 3,577,690.52 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 2,782,648.18.
No comments:
Post a Comment